Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Alexandre Leveque aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili kushoto ni Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na ofisa dawati Bi Upendo Mwasha. Picha na Ikulu
Burhan awekewa vikwazo na Marekani
8 hours ago
Post a Comment