WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na Mashirika ya nchi za nje namna wanavyopambana kuzuia na
kupunguza maambukizi virusi vya Ukimwi kwa nchi za Afrika hususani Tanzania.
Mwito huo ulitolewa na Mkuu wa Kituo
cha Afya na Maendeleo kwa ajili ya Watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi(SHDEPHA) Mkoa wa Mbeya Olivia Mahenge wakati akimkaribisha Balozi wa
Marekani nchini Tanzania Alphonso Lenhardt alipotembelea kituo hicho kilichopo
Sae Jijini Mbeya.
Alisema Watanzania wako mstari wa nyuma
katika kuiga juhudi zinazofanywa na watu kutoka nchi za Ulaya namna
wanavyopambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Maleria kwa vitendo.
Katika risala yao kwa Balozi huyo
walisema Shdepha Mkoa wa Mbeya imepata mafanikio makubwa kutoka Msaada wa Watu wa Marekani ambapo Balozi
ameshatembelea kituo hicho kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza alitembelea
Mwaka 2009.
Walisema mbali na kutoa huduma na ushauri
kwa waathirika juu ya kujikinga na maambukizi mapya pia hufanya shughuli ndogo
ndogo kama ufugaji, kilimo na Ujasiliamali ambapo hutengeneza Sabani na Chaki
pamoja na Vitambaa.
Hata hivyo walisema kuna changamoto
ambazo zinawakabili kama ukosefu wa Fedha za kuwekea umeme mkubwa kwa ajili ya
vifaa vya kutengenezea sabuni kutokana na umeme uliopo sasa kuwa mdogo ambapo
walisema wanahitaji zaidi ya Milioni 6.
Waliongeza kuwa katika kituo hicho kina
jumla ya watumishi ambao zaidi ya Asilimia 70 wanaishi na maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi hivyo wanaulewa mkubwa kuhusu madhara hayo ili kuwashauri wenye matatizo na wenye mambukizi.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani Nchini
Tanzania Alphonso Lenhardt aliwashukuru watanzania kwa kuendelea
kushirikiana naye na kuwaahidi
kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shdepha Tanzania hususani Mkoa
wa Mbeya.
Alisema kwa niaba ya Watu wa Marekani
wataendelea kutoa msaada kwa Mkoa wa Mbeya kuhusu mapambano dhidi ya Virusi vya
Ukimwi tokea waanze kwa Miaka Nane iliyopita na kwamba kwa sasa Programu 150
zinazohusu afya ni zaidi ya 40 zilizopo Nyanda za Juu kusini.
Aidha Balozihuyo yupo Mkoani Mbeya kwa
Ziara ya Siku mbili ambapo katika siku ya kwanza Balozi huyo alizindua Maabara
ya Kisasa ya Kimataifa ya Magonjwa mbali mbali katika Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya.
Maabara hiyo ambayo itajikita katika
ugonjwa wa Kifua kikuu imepewa kibali na Cheti kutoka Umoja wa Mataifa ambayo
itakuwa maabara ya pili kufunguliwa Mkoani Mbeya baada ya kuwepo Hospitali ya
Mhimbili Dar Es Salaam.
Balozi huyo alidai kwamba katika makubaliano
ya Ushirikiano kati yaSerikali ya Watu wa Marekani na Tanzania ya kusaidiana na
kudumisha undugu ni lazima yatekelezwe kwa vitendo kutokana na kuthamini afya
za watanzania.
Alisema tangu Mwaka 2008 Serikali ya
Marekani imekuwa ikishirikiana na kukubaliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii ya Tanzania kuhakikisha inatoa msaada wa kiafya kwa Watanzania kupitia
Mpango wa dharula wa Raisi wa kupunguza makali ya Ukimwi uliofadhiliwa na Watu
wa Marekani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali
ya Rufaa ya Mbeya Dk. Eliuter Samky aliwashukuru watu wa Marekani kwa kuendelea
kutoa misaada katika Mkoa wa Mbeya
hususani sekta ya Afya.
Na Mbeya yetu
|
Post a Comment