Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS JAKAYA KIKWETE USO KWA USO NA WABUNGE WA CCM

 

 
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya kikao cha siku mbili na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujadili masuala mbalimbali ya taifa, ikiwamo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika majimbo yao.
Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kuwapa nguvu wabunge wake katika kueleza masuala mbalimbali, ikiwamo hatua ya Serikali kupitisha bajeti, huku miradi ya maendeleo ikisuasua katika utekelezaji kwa madai ya kukosekana kwa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kikao hicho ni cha kazi na kitakuwa kinatoa nafasi zaidi kwa wabunge kueleza masuala yanayoh
usu utekelezaji wa Ilani ya CCM katika majimbo yao.
Nape alisema kikao hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na matukio yanatokea bungeni hivi sasa, bali ni ratiba ya kikao cha kazi za Mwenyekiti katika kupima utekelezaji wa ilani na miradi ya maendeleo katika majimbo mbalimbali ambayo yapo chini ya wabunge wa CCM.
“Hiki ni kikao cha kazi, ninapenda kueleweka kuwa CCM ndiyo iliyokabidhiwa jukumu la kuongoza nchi hii na wabunge wa chama chetu ndiyo wanaisimamia ndani ya Bunge, hasa katika kuhoji masuala mbalimbali yanayohusu nchi na watu wake. 
“Lakini kutokana na hali hii, kikao hiki kitakuwa cha siku mbili ambako siku ya kwanza itakuwa ni fursa kwa wabunge kusema masuala mbalimbali dhidi ya serikali yao.
“Kikao kitafanyika Mei 18-19 mwaka huu na wabunge watakuwa na uhuru wa kusema jambo lolote mbele ya Mwenyekiti wao.

“Katika siku hiyo ya kwanza itakuwa ni fursa kwa wabunge kusema masuala mbalimbali ambayo wanahisi ni muhimu kwa chama chao.
“Baada ya maelezo hayo, Mwenyekiti atakuwa akisikiliza na atakuja siku ya pili kwa ajili ya kutoa majibu kwa wabunge pamoja na hatua mbalimbali za kuchukua na ajenda kubwa ni ushauriano baina ya wabunge na serikali yao.
“Tunapenda kueleza jamii na Watanzania kwa ujumla kuwa CCM hivi sasa imefanya mambo kadhaa, hasa katika kuhakikisha inaisimamia vema Serikali yake, ikiwamo katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambayo ndiyo mkataba kati ya Serikali na wananchi. 
“Ni wazi kabisa hivi karibuni kuna matukio yaliyotokea bungeni, likiwamo lile la Mbunge wa Nkasi Kaskazini.
“Kikao hiki hakina uhusiano kabisa na jambo hilo, bali ni kuwakutanisha pamoja wabunge wetu ili nao waweze kutoa madukuduku yao mbele ya Rais hasa katika utekelezaji wa ilani ya chama chetu,” alisema.
Nape alisema kwa muda mrefu wabunge wamekuwa wakilalamikia hatua ya serikali kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kutokana na madai ya fedha kutopelekwa kwa wakati kama ilivyoamulia kwa Bunge.
“Ni wazi kabisa siku zote Katibu Mkuu wetu Abdulrahman Kinana amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mawaziri wanawajibika kwa moja kwa moja kwa chama na si vinginevyo, kwani upimaji wa ilani hupimwa na chama kwa kupata taarifa za utekelezaji wake wa kina,” alisema Nape.
Mgombea ubunge Chambani
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi alisema aliweka wazi uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichoketi Mei 14, mwaka huu ambacho pamoja na mambo mengine kilipitisha jina la mgombea ubunge katika jimbo la Chambani.
Alisema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemteua Mattar Sarahan Said kuwa mgombea wake wa ubunge katika jimbo hilo katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Nape alisema CCM imewateua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Idd kuzindua kampeni hizo na Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi atafunga kampeni hizo.
Bomu Arusha
Alisema mbali na hatua hiyo, Kamati Kuu ilipokea taarifa za tukio la mlipuko wa bomu Arusha na kuridhishwa na hatua za haraka zilizochukuliwa na serikali kwa kuitaka iwe inatoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi kutokana na uzito wa jambo hilo.
“Kamati Kuu ilipokea taarifa ya serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuhusu tukio la bomu Arusha na kutokana na maelezo ya Serikali, CC imeagiza hatua zaidi zichukuliwe kuhusu tukio hili, ikiwamo kung’oa mzizi wake kabisa kuweza kulinda amani na mshikamano wa nchi yetu.
“Ninajua kuna baadhi ya vyama hivi sasa tayari vimeshatoa matamko kuitaka serikali iombe radhi … lakini kwa hivi sasa si sahihi hata kidogo, ndiyo maana sisi CCM tunasema kuwa tuvute subira kwanza kwa kuiachia serikali jambo hili hadi mwisho kuliko kufanya hivyo,” alisema Nape
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top