Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UFAFANUZI WA TAARIFA MBALIMBALI ZILIZOTOLEWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI DHIDI YA DAWA BANDIA YA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI YENYE JINA LA BIASHARA TT-VIR 30 TOLEO NAMBA 0C.01.85

 

 
Hussein-Mwinyi Tarehe 9 Mei, 2013, Mhe. Dkt. Hussein A. Mwinyi (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, katika kuhitimisha hoja ya bajeti ya Wizara alitolea ufafanuzi suala la dawa bandia ya ARV kufuatia hoja zilizokuwa zimetolewa na Mhe. Zarina S. Madabida (Mb) kuhusu kuhusika kwa kiwanda cha dawa chaTanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) katika sakata la dawa bandia ya ARV.
Baada ya ufafanuzi huo wa Mhe. Waziri kutolewa, kumekuwa na taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zinazoleta mkanganyiko kwa wananchi kuhusu suala hili.
Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.  Aidha, kama ilivyoelezwa katika taarifa mbalimbali za umma zilizokwisha kutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na  TFDA  kuhusiana na suala hili, bado inasisitizwa kwamba kampuni ya TPI Ltd iliiuzia Bohari  ya Dawa (MSD) dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.
Tunapenda kusisitiza kwamba, Mhe. Waziri katika hotuba yake hakukanusha kuwa kampuni ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia bali alieleza kwamba uchunguzi wa awali katika kiwanda cha kampuni hiyo haukuonesha dawa hiyo ilizalishwa na TPI Ltd  bali vifungashio ni vya TPI Ltd na nyaraka zinaonesha TPI Ltd kuiuzia MSD dawa hizo bandia. Aidha, alieleza kuwa vyombo vya usalama bado vinaendelea kulichunguza suala hilo ili kubaini chanzo na wahusika wakuu wa dawa hizo bandia.
Kwa kuzingatia unyeti wa suala hili, Wizara inatoa wito kwa vyombo vya habari kusubiri hatma ya uchunguzi unaofanywa na vyombo vya usalama na kuepuka kutoa taarifa ambazo zinaweza kupotosha umma na jitihada kubwa za Serikali katika kupambana na dawa bandia nchini.
N. Mwamwaja
MSEMAJI
16 Mei, 2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top