Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZINAZINGATIA VIWANGO VYA TBS


 
imagesWATANZANIA  wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa na wawekezaji wazawa kwa ajili ya kukuza patato la taifa na kupanua wigo wa ajira kwa vijana nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Msambazaji wa kiwanda cha ‘Soap Industries Lmt’ Chisha Gimbi, alisema bidhaa zinazozalishwa hapa nchini hazina tatizo kwa kuwa zimezingatia vigezo vyate vya TBS.

 Alisema Watanzania hawapaswi kuendekeza tabia ya kuthamini bidhaa kutoka nje wakati vipo viwanda vya wazawa vinavyotengeneza bidhaa hizo kwa ubora wa hali ya ujuu tofauti na hizo zinazotoka nje.

Gimbi alisema kiwanda hicho ambacho kimetoa ajira kwa wazawa wapatao 270, hata hivyo alisema jitihada zao hizo zitafanikiwa endapo kasi ya watanzania itaongezeka katika kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa zao.

Alisema licha ya kutoa ajira hizo kwa wazawa bado kimeeleza masikitiko yake kwa serikali hasa kwa kutokuwa na mazoea ya kutembelea kiwanda hicho na vingine ili kubaini changamoto kadha wa kadha zinazowakabili.

 “Serikali iweke utaratibu wa kutembelea viwanda vya  wawekezaji ambao ni wazawa ili kubaini changamoto zinazowakabili badala ya kutoa fursa kwa wageni’alisema Gimbi.

Gimbi alisema kitendo cha serikali kuendelea kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa nje kimekuwa kikiwakosesha hali ya kujiamini katika kile wanachobuni.

“Ni wakati sasa kwa viongozi wa serikali, hasa waziri husika kutembelea viwanda vya wazawa  huko ili kubaini changamoto zinazotukabili na kuweka utaratibu wa kutusaidia  katika nyanja mbalimbali” anasema Chisha.

Alitoa wito kwa serikali kuamzisha mpango mkakati wa kuongeza hamasa ya mawazo itakayosaidia kukuza uchumi endelevu jambo ambalo litakalosaidia kuwaletea maendeleo Watanzani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top