Mkuu wa Mkoa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu.
Matrekta yakiwa kazini kuchimba makaa ya mawe katika Kijiji cha Mtunduwalo,kata ya Rwanda Wilaya ya Mbinga – Ruvuma | . |
…………………………………………………………………………………….. |
MKUU
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amelazimika kuufunga kwa muda mgodi wa
makaa ya mawe wa kampuni ya TANCOAL baada ya wananchi wa kijiji cha
Mtunduwalo kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga kumtaka aufunge mgodi huo
mpaka watapolipwa madai yao ya muda mrefu ya fidia pamoja na kuyaweka
mazingira yao katika hali inayostahili kwa matumizi ya binadamu.
Mwambungu
alichukuwa uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya msingi Mtunduwalo ambao ulihudhuriwa na mamia ya
wanakijiji hicho wakiwemo viongozi wa kamati za ulinzi na usalama za
Wilaya ya Mbinga na Mkoa pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Mapema
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akimkaribisha Mkuu wa Mkoa
Mwambungu ili aweze kuongea na wananchi kuhusu mgogoro uliopo kati ya
wananchi na mwekezaji wa mgodi huo ndipo alipoanza kwa kusema wananchi
wa Mtunduwalo hoyee!wananchi wakajibu hoiiii!mpaka kieleweke kadhalika
kwa mkuu wa Mkoa ambapo aliwataka kuwa watulivu wakati anapotaka
kuwaambia nini serikali yao imefanya katika kulimaliza tatizo hilo.
Pamoja
na Mkuu wa Mkoa kujaribu kuwatuliza wanakijiji hao lakini bado hali
iliendelea kuwa mbaya baada ya wananchi hao kumshinikiza mkuu huyo wa
Mkoa waende nae mpaka kwenye eneo la mgodi akaufunge na kama
haitawezekana basi wapo tayari kufa kwa kupigwa risasi kuliko kufa kwa
njaa wakati haki zao zipo zinadhurumiwa na viongozi wa serikali huku
baadhi yao wakiugua magonjwa mbalimbali kutoka kunywa maji yenye
chembechembe ya sumu ya madini ya makaa yam awe yanayochimbwa eneo la
kijiji hicho.
Akitoa
kero mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwambungu mwananchi Erick Mapunda alisema
kuwa wamechoka na ahadi hewa za mwekezaji ambazo kila kukicha imekuwa ni
siasa hivyo ujio wa Mkuu wa Mkoa huyo uwe ni hitimisho la kwenda
kuufunga mgodi huo mpaka hapo watapotimiziwa ahadi walizoahidiwa pamoja
na kuwalipa fidia wanazoidai kampuni ya TANCOAL.
Joseph
Messa alieleza kuwa yeye kama mwananchi wa kijiji hicho ameshakata tama
ya maisha kwa sababu hali ya kijiji chao ni mbaya kutokana na
kukosekana kwa miundo mbinu ya barabara,maji,shule pamoja na zahanati
kwani watoto wao wamekumbwa na magonjwa ya kichocho ambayo hawajui
yanasababishwa na nini na kwamba wamekuwa wakinywa maji ya sumu tangu
mgodi huo uanze kufanya kazi licha ya kuwa malalamiko hayo walishapewa
viongozi wa serikali ya kijiji,Wilaya na Mkoa.
Kwa
upande wake Benedina Komba alisema kuwa tangu mgodi huo uanze kufanya
kazi wananchi wa kitongoji cha Nkaya walipewa ahadi ya kuhama maeneo yao
kwa muda kwa madai kuwa wataonyeshwa maeneo mengine ambayo wangepewa
fidia ili wakajengee mahali pengine jambo ambalo mpaka sasa
halijatekelezeka huku wakiangaika na watoto kutokana na njaa kwa kuwa
eneo walilokuwa wakilima kuchukuliwa na kampuni hiyo.
Wosteri
Mapunda alielekeza shutuma nzito kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa
Ruvuma kwa kutoandika habari za mgogoro huo tofauti na waandishi wa Mkoa
wa Arusha ambao wamekuwa wakiandika habari za mgogoro wa Loliondo
ambapo serikali baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari ilihamia
Loliondo ili kumaliza tatizo lililopo na kwa nini Mtutunduwalo
ishindikane kwa muda wa miaka mitatu sasa.
Aidha
Johoni Nyimbo alimnyooshea kidole Mbunge wa jimbo la mbinga mashariki
Gaudensi Kayombo na kumkumbusha ahadi aliyowaahidi wananchi wa kijiji
hicho mei 19 mwaka 2011 kwenye mkutano wa hadhara kuwa endapo wanakijiji
hao hawatalipwa fidia wanazodai atajiuzuru nafasi aliyonayo ya ubunge
na kumtaka ajiuzulu nafasi ya ubunge mara moja jambo ambalo
lilimpandisha hasira na baada ya kauli iyo alilazimika kusimama ili
kutoa ufafanuzi wa kauli yake hali ambayo isababisha kuwapandisha hasira
wananchi hao na kuanza kumzomea.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa
halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Oddo Mwisho naye alikumbwa na adha ya
zomea zomea hiyo baada kusimama na kuanza kujieleza kuhusiana na
jitihada za chama cha CCM na Serikali yake ya Wilaya na Mkoa kuwa kwa
muda mrefu wamekuwa wakifanya mazungumzo kupitia Wizara ya nishati na
madini,Shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) pamoja na mwekezaji wa
kampuni hiyo ya TANCOAL kwa lengo la kumaliza mgogoro uliopo kati ya
mwekezaji na wananchi.
Kufuatia
vurugu zilizojitokeza kwenye mkutano huo mkuu wa Mkoa Mwambung
alilazimika kusitisha mkutano huo kwa muda na kuwataka wananchi hao
warudi eneo la mkutano baada ya nusu saa ili apate nafasi ya kujadiliana
na kamati yake ya ulinzi na usalama na baadae baada ya nusu saa kupita
mkutano ulianza ambapo Mkuu wa mkoa Mwambungu aliwaeleza wanakijiji hao
kuwa amesikia maoni yao na amefikia hatua ya kuufunga mgodi huo kwa muda
hadi hapo madai yao mbali mbali yatakapofanyiwa kazi na kutekelezwa.
Chanzo:www.demashonews.blogspot.com
Post a Comment