Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

REDD's MISS TANZANIA YAISHUKURU JAMII


 

MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency na Mratibu wa shindano la Urembo la Redds Miss Tanzania 2013, Hashim Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Itifaki, Oscar Makoye na Meneja wa Kinywaji cha Redd's, Victoria Kimaro.
Meneja wa Kinywaji cha Redd's Victoria Kimaro akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency na Mratibu wa shindano la Urembo la Redds Miss Tanzania 2013, Hashim Lundenga ameishukuru jamii kwa kuyaunga mkono mashindano hayo hali inayopelekea ubora na kuongezea heshima Taifa.

Lundenga alisema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akiongea na wandishi wa habari juu ya mwelekeo wa mashindano hilo hatua ya awali ya Vitongoji na Wilaya ambazo zinatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Mei.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wadau wa sanaa ya urembo, kuwa hatua ya ngazi ya vitongoji na wilaya yalishaanza kwa nchi nzima na tayari baadhi ya maeneo wamshamaliza
mashindano hayo na maeneo mengine yakitarajia kumaliza mwisho wa mwezi huu, tunashukuru kwa kuyapokea” alisema Lundenga.

Na kuongeza kuwa, kutokana na muamko huo, kwa mwaka huu kutakuwa na mikoa 24, inayofanya mashindano hayo, ambapo kuna Kanda 11,Vyuo vya Elimu ya juu 17, Wilaya 18, huku vituo vya Mkoa wa Dar e Salaam vikiwa 11, vyote kwa pamoja vinafanya idadi ya vituo zaidi ya 80.

Kwa hatua hiyo, Lundenga alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya awali, Mashindano ya Kanda yataanza katikati ya mwezi Juni na kuingia katika hatua inayofuata.

Kwa hatua hiyo pia, Lundenga aliwashukuru wazazi na walezi ambao wamewaruhusu watoto zao wasichana kujitojkeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original , Victoria Kimaro alisema kupitia kinywaji chao bora hapa nchini cha Redds, kimedhamiria kuhakikisha mashindano hayo yanaendelea kuwepo kwa ubora na kuendelea kutoa udhamini kwa ngazi zote.

“Tumeendelea kutoa udhamini katika ngazi mbalimbali kuanzia kitongozi hadi Kitaifa, hivyo ili mashindano kuwa bora ni vyema warembo wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kunogesha na kuongeza ushindani nah ii italeta mapinduzi makubwa katika tasnia hii ya urembo” alisema Kimaro.

Aidha Kimaro aliwaomba wadau kuendelea kukiunga mkono kinywaji hicho ili kuweza kupata nguvu ya kuwaletea burudani.

Fainali hizo zitakazofanyika siku ya Ijumaa Mei 17 katika sehemu mbalimbali ikiwemo Redds Miss Moshi Mjini, Redds Miss Kibaha,Redds Chuo cha Ustawi wa Jamii, Redds Miss Ubungo, na Redds Miss Mzizima.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top