Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga.
Ndugu
wananchi,
Jumatano
tarehe 5 Juni, 2013 Watanzania tutaungana tena na mataifa mengine kuadhimisha
Siku ya Mazingia Duniani. Siku ya tarehe 5 Juni iliamuliwa kuwa
Siku ya Mazingira Duniani kwa Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972
ikiwa ni kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Mazingira uliofanyika huko Stockholm, Uswidi.
Aidha,
Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani,
yaani UNEP, pia lilipitishwa siku hiyo. Kama mnavyojua, UNEP ni chombo pekee cha
Umoja wa Mataifa chenye makao makuu yake katika bara la Afrika, huko Nairobi
Kenya. Tangu tarehe 5 Juni, 1973, nchi mbalimbali zaidi ya 140 huadhimisha siku
hii kila mwaka.
Lengo letu
kubwa katika kuadhimisha siku hii kama Taifa ni kuweka msisitizo katika masuala
ya mazingira na kuwapa uwezo wananchi ili wawe mawakala wazuri wa maendeleo
endelevu. Vile vile maadhimisho haya hutoa nafasi muhimu ya
kutafakarikuhusu hali na umuhimu wa mazingira kwa nchi yetu, kuelimishana na
kukuza ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za hifadhi na usimamizi wa
mazingira yao.
Maadhimisho
ya Siku ya Mazingira Duniani kitaifa kwa mwaka huu yatafanyikia Mkoani Rukwa, na
kimataifa yatafanyikia nchini Mongolia.
Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Mazingira Duniani ni:
“Fikiri, Kula: Hifadhi Mazingira” au
kwa lugha ya Kiingereza ”Think – Eat – Save”. Ujumbe huu unatukumbusha na
kutuhimiza tutimize wajibu wetu ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa shughuli
tunazofanya za uzalishaji mali na utoaji wa huduma zinakuwa rafiki wa mazingira
na zisiwe chanzo cha uharibifu wake. Hapa nchini
ujumbe unaoongoza maadhimisho ya mwaka huu ni “Fikiri,
Kabla ya Kula: Hifadhi Mazingira”
Ndugu
wananchi,
Madhumuni
yangu leo ni kuwaombeni wananchi wote kuienzi Siku ya Mazingira Duniani kwa
kufanya yafuatayo:-
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kufanya
usafi kwenye maeneo ikiwa ni pamoja na kufagia na kuzoa taka na kuzitupa kwenye
maeneo yaliyotengwa, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kufyeka
vichaka vinavyozunguka makazi
yetu, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kuchimba
vyoo vya kudumu na kuvitumia, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kuzibua
mifereji na mitaro ya maji
taka, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kufukia
madimbwi ya maji, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Palipo na
mvua na maji ya kutosha, kupanda nyasi na miti inayofaa kwenye maeneo
yanayotuzunguka hasa yale maeneo
kame, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kusafisha
visima na vyanzo vya maji, <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kusafisha
maeneo ya maji kwa ajili ya mifugo,
na <!--[endif]-->
<!--[if !supportLists]-->Þ
Kutoa zawadi
kwa washindi wa mashindano ya usafi wa miji na majiji chini ya utaratibu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii. <!--[endif]-->
Ndugu
wananchi,
Katika
kutekeleza hayo niliyoyataja, wananchi mnayo nafasi ya kuchagua aina ya mchango
wa ushiriki wenu katika sherehe hizi, na namna mtakavyoona inafaa kuutoa.
Vile vile napenda kutoa wito kwenu wananchi wote mnaoishi
mjini na vijijini, mashirika ya umma, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya
kiserikali, sekta binafsi, viwanda na taasisi za elimu na utafiti kushiriki
katika maadhimisho haya katika maeneo yenu. Jukumu la hifadhi na
usalama wa mazingira ni letu sote, wazee kwa vijana, wake kwa waume.
Mafanikio yatatagemea juhudi za kila mmoja wetu anavyoshiriki katika
shughuli za kuhifadhi mazingira. Natoa wito kwamba, kuanzia tarehe
1 hadi 4 Juni, ziwe ni siku mahsusi kwa ajili ya kufanya shughuli za usafi
na shughuli nyinginezo zinazolenga kulinda na kuhifadhi ya
mazingira ya makazi yetu, mitaa inayotuhusu, vijiji vyetu, miji na majiji
yetu.
Baada ya
kusema haya, napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru sana wale wote ambao
wamejipanga kutekeleza shughuli mbalimbali za kuadhimisha Siku ya Mazingira
Duniani. Naushukuru uongozi wa mkoa wa Rukwa, kwa kukubali kuwa
mwenyeji wa maadhimisho haya kitaifa. Pia nazipongeza Halmashauri
za wilaya na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi na wananchi wote kwa ujumla
kwa ushirikiano wanaouonesha katika maandalizi ya maadhimisho haya.
Post a Comment