Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi (katikati) akiwa pamoja na Katibu wake, Mchungaji Palemo Massawe (kulia) na Ofisa Habari wa Taasisi hiyo, Sailas Malula, wakionesha mfano wa hundi ya Shilingi Milioni moja ambayo wanataraji kuikabidhi Hazina kwa ajili ya kununua ndege mpya ya serikali. Taasisi hiyo ambayo hujishughulisha na maombi imewaambia wana habari kuwa imeamua kuendesha zoezi hilo kwa ajili ya kununua ndege mpya ya Rais, kutokana na aliyonayo kwa sasa kukosa hadhi ya Rais.
Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana kuhusu adhma yao ya kuanzisha zoezi la kuchangisha fedha ya kununulia ndege mpya ya Rais. Kushoto ni Ofisa Habari wa Taasisi hiyo, Sailas Malula. Picha na Father Kidevu
Post a Comment