Mkurugenzi wa Misa-Tan Bw. Tumaini Mwailege.
Mahmoud Ahmad Arusha
Waandishi wa habari hapa nchini wametakiwa kuunganisha nguvu zao sanjari na kupaaza sauti zao katika kudai haki ya uhuru wa kazi zao na usalama wawapo kazini pamoja na suala zima la maslahi ya wanataaluma hao.
Hayo yapo kwenye tamko la waandishi wa habari hapa nchini wakati wakielekea kusherehekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani inayoadhimishwa kote duniani leo itakayoenda sambamba na Kongamano kwa wahariri na waandishi wa habari hapa nchini na kufanyika jijini Arusha.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Misa-Tan ambaye ndiye mwenyekiti wa sherehe hizo Tumaini Mwailege alisema kuwa waandishi wa habari wasipoungana na kudai haki zao hakuna wakuwasemea hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kujiangalia,na kujitathmini wapi aliposimamia.
Mwailege amesema kuwa kongamano hilo litawashirikisha wadau wote wa habari hapa nchini wakiwemo waajiri,wahariri,waandishi wa habari kutoka kwenye vilabu vyote hapa nchini,pamoja na serekali,na kuwa watajadili changamoto mbali mbali zinazowakabili waandishi wa habari.
‘’Waandishi wa habari mbali mbali kutoka hapa nchini na nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki wamealikwa kushiriki kwenye sherehe hizo zitakazo zinduliwa na Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Balozi Richard Sezibera”alisema Mwailege.
Nae Katibu wa Jukwaa la Wahariri Neville Meena amesema kuwa uhuru wa vymbo vya habari hauwezi kuachwa hvi hivi bila ya kuuzungumzia kwani kumekuwapo na changamoto mbali mbali kwa waandishi kuumizwa wakiwa kazini maslahi ya wanahabari umoja na mshikamano wao hivyo kila mwanahabari anawajibu wa kuuzungumzia kwa vitendo na kuacha kuwa watumishi wa wachache huku walio wengi wakiendelea kuumia kwa maslahi binafsi.
Siasa zisiendeshe maisha ya wanahabari wakaacha kujadili taaluma zao na maslahi yao sanjari na usalama wao wakiwa kwenye maeneo ya kazi zao tusipounganisha nguvu hakika tutakuja kuishia kuwa tegemezi kwenye taaluma hii na watu kutuona kama vyombo vya kutumiwa kwenye mikakati yao ya kisiasa badala ya kujali umma wa Taifa letu.
Post a Comment