Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima
ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es
Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya
Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi
maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika
Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli
hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka
sasa.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza
kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa
kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa
ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
CHANZO MICHUZI BLOG
Post a Comment