Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Ndugu Justine Peter Mwandu (kushoto). (Picha na Maktaba).
********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Justine Peter Mwandu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, 03 Mei, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili 28, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Justine Peter Mwandu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika hilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013