Viongozi
wa serikali ya Tanzania na Marekani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Alfonso Lenhardt (kulia) wakionyesha nyaraka mbili za Mpango
wa kukabiliana na maradhi ya mafua ya ndege. Nyaraka hizo zinahusisha
vikosi vya jeshi na raia nchini Tanzania na Kamandi ya Jeshi la
Marekani la Kupambana na Majanga Barani Afrika (USAFRICOM). Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na
viongozi mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka
Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam.Pamoja na mambo mengine
amesema Tanzania inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na
majanga mbalimbali.
Balozi
wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt akiongea na viongozi
mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka Tanzania na
Marekani leo jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa serikali ya
Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania na nchi nyingine katika
kukabiliana na majanga yanayotokea.
Washiriki
wa vikosi vya kupambana na majanga kutoka Tanzania na Marekani
wakiangalia moja ya filamu inayoonyesha athari za virusi vya mafua ya
ndege kwa binadamu iliyowahi kutokea katika moja ya nchi na hatua
zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo isilete maafa zaidi.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano huo wa siku mbili kutoka Tanzania wakifuatilia
masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha akitoa
ufafanuzi kwa waandishi kuhusu utayari wa Tanzania katika kukabiliana na
majanga mbalimbali yanayotokea kwa kuvishirikisha vikosi vya ulinzi na
usalama, wataalam wa sekta nyingine, utoaji wa tahadhari mapema kwa
wananchi na uimarishaji wa kitengo cha maafa nchini.
Washiriki
wa mkutano wa siku 2 unaojadili namna ya kukabiliana na majanga
mbalimbali na athari za Virusi vya mafua ya ndege wakiwa katika picha ya
pamoja leo jijini Dar es salaam.
Post a Comment