KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa
mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa
ujumla kuwa muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja hadi
Julai 31, 2013.
Pamoja
na nyongeza hii ya muda, Bodi inasisitiza waombaji kujaza fomu za
maombi ya kwa njia ya mtandao (OLAS) kwa usahihi na kuzingatia muda wa
maombi uliowekwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Waombaji wa mara
ya kwanza wahakikishe wanajaza kwa ufasaha na kuweka viambatanisho vyote
muhimu ili kufanikisha mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo.
Kundi
la kwanza la wanafunzi waliopangwa kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) ambao wamemaliza mafunzo hayo mwezi Juni, 2013 wanapaswa kutumia
fursa hii kujaza fomu za maombi ya mikopo bila kukosa. Aidha, kundi la
pili la wanafunzi wanaotegemea kuanza mafunzo hayo mwezi Julai, 2013
walitakiwa wawe wameshaomba mikopo kati ya tarehe 1 Mei, 2013 na 30
Juni, 2013 lakini endapo kuna wachache ambao hawakuweza kufanya hivyo
basi nao watumie muda huu wa nyongeza kujaza fomu za maombi kwa njia ya
mtandao wakiwa huko huko JKT.
Endapo
mwombaji yeyote atakabiliana na matatizo wakati wa kujaza fomu yake
anashauriwa kupiga simu kwenye dawati la huduma kwa wateja kwa namba 022
550 7910 kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 2.00 usiku siku za Jumatatu
hadi Ijumaa, na kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 10.00 jioni siku za
Jumamosi.
Ikumbukwe
kwamba Bodi haitaongeza muda wa ziada baada ya Julai 31, 2013 ili kutoa
nafasi kwa Bodi kuendelea na mchakato wa uchambuzi na upangaji mikopo.
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Post a Comment