Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi
akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al
Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma
jana.
Kaminisha wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe.
Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin
Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Dodoma jana.
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu
wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid
Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma
jana.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara
baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya
kibunge ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge
haya mawili.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika
wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini
mikataba ya makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman
na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania.
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

Post a Comment