Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote
kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara
ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya
Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013.
Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache.
Aidha
uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo
waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo.
Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda
wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia
Jumanne Juni 25, 2013.
Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam
Nujoma, Mwenge
S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: +255 22 2669036/2669037 Faksi: +255 22 2669039
Barua pepe: info@heslb.go.tz
Tovuti : www.heslb.go.tz
Post a Comment