Katibu wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana
wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora
mjini.
Mbali ya
Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage
wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, leo
wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika
kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa
hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la
pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.
Kesi hiyo
ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora
Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma
Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya
kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah
Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba
mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza
mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa
Mashtaka nchini.
Sheria za
uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama hayo
yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo. Kwa kuwa
ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia mbali kesi
hiyo.
Sababu ya
pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi kuwa ni ya
ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na makosa mengine ya
kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo waliiomba Mahakama kutupilia
mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa la kawaida.
Na sababu
ya tatu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, sheria inaelekeza
kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye mamlaka na hadhi kama ile
waliyopelekwa katika maeneo yale walikokamatwa. Hivyo mawakili waliiomba
mahakama itupilie mbali shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia
walipaswa kushitakiwa katika maeneo yao walipokamatwa. Baada ya hoja hizo,
Mahakama iliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Julai 8 mwaka huu Tabora
Mjini.
Hii sio
mara ya kwanza kwa viongozi au wafuasi wa chadema kufunguliwa kesi zinazohusiana
na ugaidi, tarehe 18 Machi 2013, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare, la Ludovick Joseph walifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na
mashtaka manne yakiwemo ya ugaidi.
Kosa
jingine lililowakambili Lwakatare na Ludovick ni kula njama; kosa ambalo pia
linawakabili washtakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria
ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka
2002.
Katika kosa
la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kufanya mkutano wa kupanga kufanya
makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia
ugaidi.
Wakili wa
serikali alidi kuwa washitakiwa wote Desemba 28 Mwaka jana walishiriki katika
mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara Msaki kinyume na kifungu
4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.
Pamoja na
tuhuma hizo, 8 Mei, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia mashitaka
matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Katika
uamuzi huo Jaji Lawrance Kaduri akitoa uamuzi huo alisema ulitokana kukubaliana
na hoja ya mawakili wa Lwakatare; Tundu Lissu, Peter Kibatara na Mabere Marando
na kusema kuwa.
“Baada ya
kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama inatoa amri ya kumfutia Lwakatare
mashitaka matatu, yaani kosa la pili, tatu na la nne kwa sababu Jamhuri
imeshindwa kuonesha maelezo yanayotesheleza kumshitaki Lwakatare kwa kesi ya
ugaidi.
“Naamuru
jalada la kesi ya msingi lilirudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya mshitakiwa
kuendelea kushitakiwa kwa kosa moja la kula njama ambalo linaangukia katika
sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002,” alisema Jaji Kaduri
Imechotwa: Habari Mseto Blog
Post a Comment