WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu
kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na
tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa
mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni
ya kuwakomboa vijana.
Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha
kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine
nchini.
“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge
mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni
cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.
Lowassa alisema tatizo la
ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana
na tatizo hilo amani itatoweka.
“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya
uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya
Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.
Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni
wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo,
sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh
milioni 10 na pikipiki 10
Loading...
Post a Comment