Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali
ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake
ya Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka
mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita
wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam
kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa
Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687
wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali,
ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23,
ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha
ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia
itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya
deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu
iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za
aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani
mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili
hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani
kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina
zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya
Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa
kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.
Post a Comment