Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FOLENI KIKWAZO MAONYESHO YA SABASABA

Photo: Foleni kikwazo Sabasaba

Katika Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa, Barabara ya Kilwa, zinaonekana heka heka za kila aina-zikiendelea ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maonyesho ya 37 ambayo yanatarijiwa kufunguliwa kesho mpaka Julai 8 mwaka huu.

Kwenye viwanja hivyo, wapo ambao wanafyeka nyasi zilizozunguka majengo, kupaka rangi, kutengeneza bustani na pia wapo ambao wanahaha kusaka vibarua vya ujenzi na ukarabati na mwingine unaoendelea.

Mabanda yakarabatiwa

Washiriki wanaonekana wakisimamia ukarabati wa mabanda yao huku Mamlaka ya Maonyesho ya Biashara Dar es Salaam (DITF), ikitoa semina na maelekezo mengine kwa washiriki.

Maonyesho hayo ni mmoja kati ya maeneo mengine ambayo yanatajwa kuchangia ukuaji wa uchumi nchini katika sekta ya biashara na uwekazaji. Takwimu za Wizara ya Fedha zinabainisha kwamba kumekuwapo kwa maendeleo makubwa ya kiuchumi miaka ya karibuni kulinganisha na kipindi kingine.

Takwimu hizo zinabainisha kwamba uchumi umekuwa kwa asilimia 6.9 kiwango ambacho ni kikubwa kulinganisha na mwaka 2011-ukuaji ulikua kwa asilimia 6.3.

Kaimu Mkurugenzi wa DITF, Jacueline Maleko anasema maonyesho hayo mwaka huu washiriki wameongezeka ukilinganisha na mwaka uliopita. Nchi zilizothibitisha kushiriki ni 32 tofauti na kipindi kilichopita, nchi washiriki walikuwa 11.

Kampuni za nje zilizothibitisha kushiriki ni 401 kutoka wakati za ndani ni 1,000 na taasisi za serikali ni 70 hali ambayo inaonyesha wazi kuwa maonyesho ya sasa yatakuwa na fursa nyingi za biashara kuliko maonyesho yaliopita.

Mwaka huu Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (UNIDO), wametenga banda mahsusi kwa bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuleta tija kwa wajasiriamali, wakulima na wawekezaji wengine wa ndani.

Mfanyabiashara wa ngozi kutoka mkoani Kilimanjaro, Issaya Bunu anasema maonyesho ya biashara ya kimataifa ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara hasa wazalishaji wa bidhaa zmbalimbali, lakini ni wachache ambao wanayatumia vizuri.

Anasema hali hiyo pengine inatokana na elimu ndogo ya biashara, na anabainisha kwamba wengi wanachukulia ni eneo la kuuzia bidhaa, lakini kimsIngi ni sehemu mahsusi kwa ajili ya kujitangaza na kuweka miadi ya kibiashara na kutengeneza wadau katika sekta hiyo.

“Kila mwaka ninapiga hatua, nina mwaka wa 10 sasa nashiriki maonyesho haya na kimsingi natamani miaka yote siku ziongezwe kwani tija ni kubwa kuliko inavyodhaniwa,”anasema.

Anabainisha kwamba kutokana na kushiriki maonyesho hayo amepata soko la kuuza bidhaa zake katika nchi za Pakistani, China, na Uingereza.

Mdau wa biashara, Emiliana Cheyo anayachukulia maonyesho hayo kama sehemu ya kuchagua bidhaa na hata kuzitafutia masoko nje ya nchi kwani kuna vitu vingi ambavyo nje vinauzika, lakini havijapata nafasi kwenye ngazi za kimataifa.

“Nashukuru angalau kuna maonyesho ya namna hii nchini, lakini changamoto iliyopo ni kwa wafanyabiashara nchini ambao wanashiriki kwenye maonyesho kama haya katika mataifa mengine nje na hili ni jukumu la serikali” anasema.

Anabainisha kuwa serikali inatakiwa kutoa elimu na kuzitangaza fursa zilizopo nje ya nchi kwa kuwasaidia wajasiriamali kusafiri na kushiriki maonyesho ya namna hiyo na kitu kama hicho anasema kinafanywa na mataifa mengine jirani kama vile Kenya na Rwanda wanavyofanya.

Foleni kikwazo sabasaba

Maonyesho hayo yanafanyika Jiji la Dar es Salaam likiwa linakabiliwa na changamoto kubwa ya foleni za magari karibu barabara zote kuanzia asubuhi hadi jioni jambo ambalo linaweza kuwakwamisha washiriki endapo hatua hazitachukuliwa kutatua tatizo hilo.

Kukabiliana na tatizo hilo aliyekuwa Mkurugenzi wa maonyesho hayo, Ramadhan Khalfan alisema kuna haja ya kujengwa hoteli kwa ajili ya wageni kufikia ndani ya viwanja hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanalazimika kusafiri umbali mrefu huku wakikumbana na foleni isiyotembea.

Mkurugenzi huyo anasema hoteli za ufukweni zinapokea wageni wengi kutoka mataifa mengine hasa Ulaya na Marekani ambao wanakuja kwa ajili ya maonyesho hayo ya kimataifa.

Wafanyabiashara kutoka Zanzibar, Lucy Urio anasema ukosefu wa hoteli kwa wageni maeneo ya jirani huenda ukagharimu maonyesho hayo siku za mbele kwa kuwa siku za maonyesho ni chache ukilinganisha na maonyesho ya nchi nyingine zingine.

Haijulikani ni utaratibu gani utatumika wakati huu, lakini hakuna dalili ya kuwapo kwa mbinu mpya za kukabiliana na tatizo hilo na kimsingi serikali inapaswa kuisaidia Mamlaka ya Mandeleo ya Biashara (Tan-Trade) katika mapokezi na usalama wa wageni wao.

Msongamano wa magari, umbali mrefu kutoka katika maonyesho hadi wageni walipofikia ni sehemu ya vikwazo vya biashara ambavyo vinapaswa kuepukwa kwa ustawi wa maonyesho hayo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi. Kinyume cha hivyo watangazaji watakimbia.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top