Na Mwandishi wetu
Naibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashidi amesema idadi ya viziwi nchini itaongezeka hadi kufikia 24,080 mwaka 2016.
Dk. Rashidi alitoa takwimu hizo wakati akifungua
mkutano mkuu wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita) mjini hapa hivi karibuni.
Alisema idadi hiyo itaongezeka kutokana na mlipuko wa majanga mbalimbali ya asili kama vile magonjwa , ajali za barabarani na utapiamlo kutokana na lishe duni kwa baadhi ya Watanzania.
Akingua mkutano huo, alikitaka Chavita kutumia vizuri misaada ambayo wamekuwa wakiipata ndani na nje ya nchi kwa kufuata taratibu na makubaliano baina yao na wahisani.

alisemani vema wakazingatia makubaliano ya jinsi ya kutumia misaada ili kuimarisha uhusiano baina yao.
Awali akisoma risala Mjumbe wa Bodi ya Chavita, Esha Abdallah alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii kama vile afya, elimu, ajira na ushirikishwaji katika mambo ya kuichumi katika jamii.
Akizungumzia suala la afya alisema viziwi wengi nchini wamekuwa wakikosa huduma ya matibabu ama kutotibiwa kwa uhakika kutokana na kukosa mawasiliano baina yao na madaktari, wauguzi na wahusika wengine katika vituo vya afya.
Kuhusu elimu, alisema kwa viziwi ni duni kwa kukosa wataalamu wakutosha wa lugha ya alama na vifaa vya kufundishia.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment