Watoto wa nchini Afrika Kusini wakimwombea Rais Mstaafu wa nchi hiyo,
Nelson Mandela nje ya Hospitali ya Medi Clinic alipolazwa kwa matibabu.
Picha na AFP.
Baadhi ya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya Makazi yake wakimuombea. |
Matengenezo yakiendelea kufanyika. |
JOHANNESBURG:
WAKATI kukiwa na vita ya chini kwa chini dhidi ya vyombo vya habari vinavyofuatilia mwenendo wa afya ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kumekuwa na pilika nyingi katika makazi ya kiongozi huyo yaliyopo eneo la Houghton, Mtaa wa Laan 12, jijini Johannesburg.
Leo ni siku ya 22 tangu Mandela alazwe katika
hospitali ya magonjwa ya moyo, Medclinic iliopo Pretoria akiugua ugonjwa
wa figo na katika siku saba zilizopota taarifa rasmi zinasema “hali
yake ni mbaya”.
Usiku wa kuamkia jana, Mwenyekiti wa taifa wa
chama tawala cha ANC, Baleka Mbete aliongoza maombi ya kumwombea Mandela
kwa wanachama na makada wake waliopo majim
bo ya Cape Town na Eastern Cape huku akisisitiza:
bo ya Cape Town na Eastern Cape huku akisisitiza:
“lazima wananchi wa Afrika Kusini, wafike mahali wamruhusu Mandela ampumzike kwa mapenzi ya Mungu”.
Wakati hayo yakiendelea pilika katika makazi ya
Mandela ziliwahusisha makundi ya watu na kampuni kadhaa za jijini
Johannesburg, wakiwamo watu waliokuwa wakifanya usafi.
Kazi hiyo ilifanyika kwa kufagia na kuzoa taka,
usafi wa vitalu na kubadilisha mawe, utengenezaji wa bustani za maua na
pia mafundi waliokuwa wakifanya shughuli za marekebisho ya njia za umeme
katika eneo hilo.
Mmoja wa majirani katika eneo hilo
alyejitambulisha kwa jina la Jacob Brews alisema: “Huwa watu wanafanya
usafi hapa lakini ninaona kama leo kuna jambo la ziada hapa. Maana watu
ni wengi na kila mmoja anaonekana anatekeleza wajibu wake”.
Katika nyumba hiyo kulikuwa na idadi kubwa ya
magari kuliko kawaida na ilipotimu saa 6.00 mchana magari saba yalikuwa
yameegeshwa mbele ya lango la nyumba hiyo ikiwa ni ishara kwamba
wahusika wake walikuwa ndani.
Mwananchi lilishuhudia magari mengine yakiingia
ndani na kutoka kila baada ya muda, huku baadhi ya wageni wakiingia
ndani wakiwa wamebeba maua. Kabla ya jana hakukuwa na watu wengi
walioonekana wakiingia katika nyumba hiyo.
Watu wanaodhaniwa ni maofisa usalama pia walikuwa
wametapakaa nje ya makazi hayo walikuwa wakifuatilia kwa karibu
mazungumzo ya waandishi wa habari na walinzi pamoja na watu waliokuwa
wakifanya shughuli mbalimbali.
Mmoja wa walinzi hao aliliambia Mwananchi kuwa
hawezi kuzungumza chochote. “Tunafuatiliwa sana maana hawataki
tuzungumze chochote kile ambacho kinatokea huko ndani, labda kama
ungenitafuta nje ya hapa”.
Pilika zilivyokuwa. CHANZO MWANANCHI.
Post a Comment