Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

GIDAMIS SHAHANGA NDIYE MWANARIADHA MTANZANIA WA KWANZA KUWEKWA KWENYE STAMP YA TANZANIA YA MWAKA 1980.


 GIDAMIS SHAHANGA ni mwanariadha maarufu sana wa miaka ya 70 naa... hadi 1990 aliyeliletea Taifa letu la Tanzania heshima na rekodi isiyofutika katika rekodi sahihi za riadha nchini Tanzania na kote duniani.

Gidamis ndiye mwanariadha wa kwanza hadi sasa ambaye picha yake iliwekwa katika STAMP (ya barua) ya Tanzania mnamo mwaka 1980 wakati wa utawala wa Mhasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Gidamis Shahanga ni mwanariadha mstaafu aliyekuwa amejikita katika  mbio ndefu za mita 10,000 na mbio za Marathon. Shahanga alizaliwa Septemba 4, 1957 kaskazini mwa Tanzania yani Katesh Wilayani Hanang Manyara.

 Kutoka kushoto (25) ni Zacharia Barie (Mtanzania) na katikati (26) ni GIDAMIS SHAHANGA wakimuonyesha umahiri mkenya (23) katika mbio zilizofanyika San Juan Porto Rico miaka ya 1980.

 Ni vyema serikali na wadau wa michezo nchini kuwaenzi wachezaji wa zamani walioliletea Taifa letu heshima katika michezo mbali mbali hapa nchini kama Gidamis Shahanga. Kwa pamoja tunampongeza sana bwana Gidamis Shahanga kwa kuonyesha ushujaa wake katika mchezo wa riadha hapa nchini miaka ya 70.

 HAYA NI BAADHI YA MAFANIKIO YAKE YA KIMATAIFA


Gidamis ni msaada mkubwa kwa wanariadha kadhaa wa hapa nchini Tanzania kama vile Wilhelm Gidabuday ambaye alifanikiwa kwenda Marekani mwaka 1993 kwa msaada wa bwana Shahanga.
GIDABUDAY (kushoto) na mwanae SYDNEY  GIDABUDAY - (kulia).

Gidabuday
anamshukuru sana Gidamis Shahanga kwani yeye ndiye mlezi wake aliyempatia elimu yani scholarship Chuo cha Riverside California ambapo pia alifanikiwa katika mchezo wa riadha. Mafanikio yake ya riadha yalimfanya ajumuike na mkewe kule nchini Marekani na kufanikiwa kupata mtoto wao wa kiume SYDNEY GIDABUDAY ambaye kwa sasa ni mwanariadha chipukizi anayefanya vizuri huko Marekani.

SYDNEY amesema kuwa
"kati ya watu muhimu nitakao watembelea katika safari yangu ya Tanzania mwishoni mwa Julai mwaka huu zaidi ya familia yangu ni GIDAMIS SHAHANGA".

SITE ya
NDGSHILATU BLOG  inawaenzi wachezaji maarufu walioliletea Taifa letu heshima katika michezo mbali mbali hapa nchini. Fuatilia shujaa wetu mwingine atakayefuata hapa hapa


credit: Asili Yetu Blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top