Hali bado ni tete
katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu
Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza
kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha
Mgomo huo.
Akisoma Tamko la
kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses
amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi
Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
Hata hivyo Kaimu
Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya
Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.
Ameongeza kuwa kama
kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi
wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya
kubatilisha.
Post a Comment