MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), Absalom Kibanda, anatarajia kuwasili nchini leo mchana. Kibanda
atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam,
saa 7 mchana, akitokea nchini Afrika Kusini, alikokuwa akitibiwa baada
ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena, ilisema baada ya kuwasili uwanjani hapo, Kibanda atazungumza na waandishi wa habari ili kuwaeleza mambo machache aliyonayo.
Kutokana na ujio huo, Meena amewataka wahariri wawapange waandishi wao katika tukio na pia wahariri wawe uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea kiongozi wao.
“Itakumbukwa, Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, amekuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu tangu Machi 6, mwaka huu, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5.
“Baada ya kuwa nchini Afrika Kusini kwa miezi kadhaa, kesho (leo) saa 7 mchana, atawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
“Baada ya kuwasili, atazungumza kwa ufupi na waandishi wa habari, kwa hiyo, naomba waandishi wa habari wawepo kwa ajili ya kutangaza kurejea kwake, lakini pia kufikisha ujumbe atakaoutoa kwa umma.
“Kupitia taarifa hii, nawaomba wahariri wote tufike uwanja wa ndege, kuanzia saa 6.00 mchana kwa ajili ya kumpokea mwenzetu huyu, ambaye amekuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
“Nasema hivyo, kwa sababu hii ni fursa nyingine adhimu ya waandishi wa habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja wetu.
“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Jukwaa la Wahariri na wahariri wote kwa ujumla, nachukua fursa hii kumkaribisha nyumbani Kibanda, ambaye kuumizwa kwake kuliitikisa tasnia ya habari nchini, pole sana Kibanda na tunakukaribisha sana nyumbani Tanzania,” alisema Meena katika taarifa hiyo.
Siku ya tukio, Kibanda alitekwa na watu wasiojulikana baada ya kumvizia alipokuwa akijiandaa kuingia nyumbani kwake, Mbezi Dar es Salaam.
Baada ya kutekwa, watekaji hao walimtoboa jicho kwa kutumia kitu chenye ncha kali, walimkata mapanga, walimnyofoa kucha za vidole na pia walimkata mapanga kichwani.
Wakati Kibanda anarejea leo nchini, mpaka sasa polisi hawajafanikiwa kukamata hata mtu mmoja, ikiwa ni siku 88 tangu alipotekwa.
MTANZANIA

Post a Comment