Wananchi wakitembeza kichapo kwa mbakaji huyo mjini Iringa leo |
Mbakaji akivuja damu baada ya kupasuliwa na mawe kichwani |
Mtuhumiwa wa ubakaji akipelekwa polisi leo |
Huyu ndie mtoto aliyebakwa na jemba hilo |
mwananchi mwenye hasira kali akimwadhibu kwa ngumi mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto mjini Iringa mchana huu.
......................................................................................................................................................
WAKATI mkoa wa Iringa ukiwa ni mkoa wa pili kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI
ukiwa nyuma ya mkoa wa Njombe ambao ndio
unaongoza huku vitendo vya ubakaji na
mapenzi yasiyo salama vikitajwa ni
sababu ,Jemba mmoja mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na
wananchi wenye hasira kali baada
ya kubambwa akibaka kitoto
cha miaka 10 mchana kweupe.
Mashuhuda wa
tukio hilo wameeleza
kuwa tukio hilo limetokea
mida ya saa8 mchana baada ya mama
mazazi wa binti huyo kusikia mtoto
wake akilia kwa uchungu kuomba msaada
zaidi kwa wananchi baada ya kukamatwa kwa nguvu na kijana huyo mbakaji
Mama mzazi wa mtoto
huyo ambae Jina lake na la mtoto
wake kwa sasa yamehifadhiwa na
mtandao huu kutokana na sababu
za kimaadili ,alisema kuwa wakati
tukio hilo likitokea
yeye alikuwa akiendelea na shughuli
zake nyumbani na kusikia sauti ya mtoto
wake akilia kwa uchungu kulalamika
kubakwa .
Hata hivyo alisema baada ya kutoka nje na
kuelekea eneo hilo ambalo sauti ilisikika alishuhudia kijana huyo akiendelea kumbaka mtoto
wake jambo lilopelekea
kupiga kelele kuomba msaada kwa wananchi ili kusaidia
kumkamata mtuhumiwa huyo wa
ubakaji.
Mwanamke huyo
alisema kuwa jitihada za wananchi
wa eneo hilo la Mwangata kumkamata
mtuhumiwa ziliweza kufanikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutaka kujaribu
kukimbia eneo hilo.
Mmoja kati ya
wananchi walioshiriki
kumkamata kijana huyo mbakaji
aliyejitambulisha kwa jina la Samweli kalinga alisema kuwa
kijana huyo amekuwa na tabia ya kuwabaka watoto
katika eneo hilo la Mwangata na mara
nyingi watoto wamekuwa
wakibakwa ila walikuwa hawajui ni nani anayeendesha vitendo hivyo vya ubakaji .
Hivyo alisema
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wa
ubakaji kulepelekea wananchi wenye hasira kali kuanza kumwadhibu kwa kichapo na hata kutaka
kumchoma moto kabla ya baadhi ya
wananchi kutumia busura na kutaka
afikishwe kituo cha polisi.
Mtuhumiwa huyo
amefikishwa katika kituo kikuu cha
polisi mjini Iringa huku akiwa hoi kwa kichapo na kupelekea kuvuja damu
kupita kiasi kichwani kutokana na kichapo alichokipata kutoka kwa
wananchi.
CREDITS: mtandao wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com
Post a Comment