Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kilimanjaro Music Awards 2013 Kuonyeshwa Live Mtandaoni


Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music  Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8. Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio  lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa
Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu
watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu
wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini. 

Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja
kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za
Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application
ya LIVESTREAM itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao  wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia
http://new.livestream.com/KTMA2013 na katika Blogs mbalimbali. 

Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbi zitapatikana kupitia
ukurasa wa Instagram wa Kilimanjaro Premium Lager ambao ni
www.instagram.com/kili_lager wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana  pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top