Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid
(wapili kushoto) katika mazungumzo maalum yaliyofanyika kwenye hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Wapili kulia
ni Katibu wa HKT ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro. Wengine, Watatu kushoto ni Balozi wa Palestina nchini, Dk. Nasri
Abujais.


Katibu
wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro,
akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO),
Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho,
alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere,
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja
naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat (Kushoto).
Wapili kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini Dk. Nasri Abujasir.
Katibu
wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro,
akizingumza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO),
Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho,
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam. Kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kuanzia saa 3.30 asubuhi, kwenye hoteli ya Protea
Courtyard, jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Post a Comment