Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus Peter Brandes,
wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo kwa
ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake, nchini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus
Peter Brandes, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es
Salaam, leo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
**********************************
Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal leo Jumatano Juni 12, 2013 amekutana na Balozi wa Ujerumani nchini
Tanzania Klaus Peter Blandes, ambaye amefika ofisini kwa Mheshimiwa
Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga.
Balozi
Blandes alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa katika kipindi chake
kama Balozi nchini Tanzania, Ujerumani imeendelea kuwa mshirika mzuri wa
Tanzania na kwamba anaamini alikuwa anaendeleza historia ya mahusiano
mema ambayo Tanzania imekuwa nayo kwa miaka mingi.
Katika
maeneo ambayo Ujerumani imekuwa katika uwekezaji Tanzania ni sambamba
na eneo la Nishati ya umeme na usafirishaji ambapo tayari makampuni
kadhaa ya Ujerumani yameonesha nia ya kuwekeza katika Reli ya Kati kwa
lengo la kufungua soko kwa nchi za Afrika Mashariki. Pia, Ujerumani ina
uwekezaji mkubwa katika sekta ya ujenzi hususani viwanda vya saruji.
Kwa
upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi Blandes kuwa
amefanya kazi nzuri katika kuhamasisha mahusiano baina ya Tanzania na
Ujerumani na kwamba katika kipindi chake akiwa Balozi hapa nchini,
uhusiano wa Ujerumani kwa Tanzania umezidi kuimarika na mchango wa nchi
hiyo katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania ni
kiashirio kizuri cha urafiki na udugu.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alimueleza pia Balozi Blandes kuwa, Ujerumani imeendelea
kuwa rafiki wa Tanzania na sasa pia rafiki wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Balozi Blandes anasema; “Ujerumani inaitazama Afrika
Mashariki kama eneo ambalo ni muhimu kwa uwekezaji na pia Tanzania inayo
maeneo mengi ambayo yanaweza kuboreshwa na hivyo kuzidisha uzalishaji
kwa soko la ndani na nje.”
Balozi
Blandes anafafanua pia kuwa, Tanzania ina mengi ya kujivunia na ni nchi
inayoheshimika sana duniani. “Mheshimiwa Makamu kama hapa kwenu
wanakuja viongozi mbalimbali wakubwa wa Dunia mnachotakiwa kufanya ni
kuendeleza pazuri mlipo ili nchi yenu ipate tija,” anasema.
Katika
mkutano huo sambamba na Balozi Blandes kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa
Rais kwa ushirikiano aliompatia katika kipindi akiwa Balozi, pia
Mheshimiwa Makamu wa Rais alimtaka Balozi Blandes kuendelea kuwa rafiki
wa Tanzania kwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi sambamba na yeye kama
Balozi aliyefanya kazi vema hapa Tanzania.
Post a Comment