Lori
lenye namba za usajiri T 382 BPE, likiwa limeangukia gari ndogo aina ya
Vtz, lenye namba za usajiri T 685 BGZ, eneo la Mbezi Tangi Bovu, jijini
Dar es Salaam jana usiku. Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa Lori
hilo lilikuwa likijaribu kuipita gari hiyo ndogo na kupanda ukuta wa
barabara na kukatika exel na kisha kuanguka na Ng'ombe wote waliokuwamo
katika Lori hilo walitawanyika huku wananchi waliowahi kusogea eneo hilo
wakianza kuswaga Ng'ombe kila mmoja akijisevia kwa wakati wake na njia
yake na hadi Kamera ya Sufianimafoto inafika eneo la tukio walikuwa
wamebakia Ng'ombe 5 tu huku wakizagaa zagaa katikati ya eneo la bustani
la barabara hiyo.
Hawa ndiyo Ng'ombe waliobaki kati ya waliokuwa wamejaa Lori hilo, hapa wakizagaa wasijue pa kwenda.
Gari
ndogo aina ya Vtz, likiwa limeegemewa na Loro hilo. Katika ajali hiyo
Kondakta wa Lori alijeruhiwa lakini Dereva wa hili gari dogo, ambaye
alikuwa ni mwanamke, alitoka mzima...............
Lori likiwa limeng'oka matairi baada ya ajali hiyo.....
Taswira ya ajali hiyo.....
Credits: Sufiani Mafoto blog
Post a Comment