Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na warembo
wanaotarajia kushiriki shindano la Redd's Miss Tanzania, 2013 wakati
alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi yanayoendelea katika Ukumbi
wa Meeda Pub. Shindano hilo linatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu
katika ukumbi huo huo.
Lundenga, akizungumza na Warembo hao leo kwenye ukumbi wa Meeda Pub.
*****************************
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa
mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, leo Jumanne jioni
alitembelea kambi ya washiriki wanaojiandaa kushiriki katika shindano la
Miss Sinza na kusisitiza hakuna rushwa ya ngono katika mashindano yao.
Lundenga
aliongozana na ujumbe wake, ambao ni Bosko Majaliwa, Katibu wa Kamati
ya Miss Tanzania, Albert Makoye Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa kamati
hiyo, Hidan Rico, Afisa wa Habari wa kamati hiyo, Yasson
Mashaka, Mkuu wa Mipango wa Kamati hiyo na Lucas Luta, ambaye ni
mjumbe.
Lundenga,
alifika Meeda Pub, ambapo washiriki wa Miss Sinza wanafanya mazoezi,
alifanya nao mazungumzo na washiriki hao kupata fursa ya kuuliza maswali
yao yaliyokuwa yakiwakwaza kuhusu tasnia ya urembo.
Akizungumza
na warembo hao, Lundenga aliwaonya washiriki hao kutojirahisi kutoa
rushwa ya ngono ili kujihakikishia nafasi katika mashindano hayo.
''Msijirahisi
kutoa rushwa ya ngono ili kupata nafasi, hata mimi nitakutafuna bure tu
au mwandaaji yeyote
atakudanganya tu na kukuacha kama ulivyo kwani mashindano haya
yanafuata taratibu zake na kanuni za mashindsano yasiyoweza kutoa fursa
kwa waandaaji kutoa upendeleo kwa yeyote'' alisema Lundenga
Ujumbe
huo uliofika kuwatembelea katika shindano hilo, uliwataka kuwa makini
kuepuka utapeli wa watu wanaowaomba ngono ili wapewe ushindi.
"Huwezi
kupata ushindi kwa kutoa rushwa ya ngono, majaji wako wengi, je utawapa
ngono wangapi ili uweze kufanikiwa kuwa mshindi. Hilo liko wazi kwamba
huwezi kufanikiwa kwa kutoa ngono," alisema Lundenga.
Naye
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa katika shindano
hilo litakalofanyika Juni 7, litasindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta,
itakayotumia fursa ya kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo
katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo
itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.
Aidha
Majuto, alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya
kwanza tokea mwaka jana mwezi julai ambapo ilitumbuiza katika
mashindano hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. Alisema kuwa hii ni
faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo
kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte
Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza.
“Ikumbukwe
kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo
kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake
katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa
Sufianimafoto.com, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com” alisema
Majuto.
Alisema
kuwa jumla ya warembo 12
wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya
waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata
nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na
baadaye Miss Tanzania.
“Tuna
warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya
urembo mwaka huu, wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo
mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika
mashindano hayo,” alisema
Post a Comment