Mwili wa marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la baba Daudi ukiwa katika gari la polisi
Huu ndio mwili wa marehemu huyo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi leo
Hapa penye damu ndipo alipopigwa risasi
Askari polisi wakiushusha mwili huo tayari kuuhifadhi chumba cha maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Majeruhi wa risasi Dismas Nyaulingo kulia na Patrick Vatung'a wakiwa wodini leo
.......................................................................................................................................
WAKATI kikao cha wadau wa ulinzi kinataraji kufanyika kesho jumanne
mkoani Iringa katika ukumbi wa Siasa ni kilimo kikao kinacholenga
kupambana na mtandao wa uharifu mkoa ya kusini mwa Tanzania ,
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi
wakiwa na silaha wamevamia maduka eneo la Zizi la Ng'ombe jirani na
msikini mjini Iringa na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili kwa
risasi kabla ya kupora fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 .
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza
mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na mtandao wa
www.matukiodaima.com baada ya kufika eneo la tukio kuwa majambazi hao
wakiwa zaidi ya wawili walivamia eneo hilo muda wa saa 1.30 usiku
wa leo .
Mashuhuda hao walisema kuwa majambazi
hao baada ya kufika katika eneo hilo la kibanda cha M-Pesa
kinachomilikiwa na Zamoyoni na kufanikiwa kumpora kiasi hicho cha
fedha kabla ya kuelekea katika duka moja wapo maarufu eneo hilo kwa
lengo la kuvamia na kupora.
Alisema Kevin Kalinga kuwa chanzo cha
kuuwawa kwa mwananchi huyo aliyetambuliwa kwa jina la baba Daudi ni
kutokana na kugoma kutii amri ya majambazi hao ambao walimkuta
akitoka dukani kununu sigara na kumtaka kukaa chini na baada ya
marehemu huyo kugoma kukaa chini ndipo walipomfyatulia risasi mwili
jirani na pega na kupelekea kutimua mbio na kujificha chini ya gari
lililokuwa limeegeshwa nje ya duka hilo gari aina ya Toyota Hilux
lenye namba T 258 .
Hata hivyo baada ya kupigwa risasi
kwa mwananchi huyo wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo walianza
kujikusanya kwa lengo la kuwavaa majambazi hao hali iliyopelekea
majambazi hao kuanza kufyatua risasi ovyo na kujeruhi wananchi
waliokuwa karibu na eneo hilo.
Kwa upande wao majeruhi wa tukio hilo
ambao wamelazwa wodi namba 5 katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa Dismas Nyaulingo ( 20) na Patrick Vatung'a(19) walisema kuwa
wao walikuwa wakiendelea kucheza Pool eneo hilo na baada ya kusikia
mlio kama wa baruti walianza kujihami kwa kukimbia na ndipo
walipokutwa na mkasa huo .
Nyaulingo alisema chanzo cha majambazi
hao kuanza kufyatua risasi onyo ovyo ni baada ya wananchi kuanza
kujikusanya kwa lengo la kupambana na majambazi hao .
"Sisi tulikuwa tukicheza mchezo wa
Pool eneo hilo na baada ya hapo tulisikia mlio wa risasi hewani na
tukajua ni baruti na baada ya kusikia mlio wa pili ndipo tulipoanza
kutimua mbio kabla ya kupigwa risasi "
Nyaulingo yeye amedai kujeruhiwa eneo
la paja lake la mguu wa kushoto huku mwenzake Vatung'a akijeruhiwa
eneo la paja la mguu wa kulia.
Madaktari waliowatibu majeruhi hao wamedai kuwa hali zao zinaendelea vizuri na uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku
chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumpandisha cheo aliyekuwa
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda ambae
kutokana na kupanda kwake kwa cheo wakati wowote kuanzia wiki hii
atauaga rasmi mkoa wa Iringa na kwenda kuanza maisha mapya katika
kiti cha enzi mpya.
CREDITS: MATUKIO DAIMA
Post a Comment