Akizungumza kwa njia ya simu jana, baba mzazi wa kijana huyo, Seni Kamera alisema mwanawe Valence Abel (23), mkazi wa Zunzuli, Shinyanga, alikuwa akiishi Kahama kwa mganga wa kienyeji, akipata matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume.
Alisema mwanawe huyo aliishi kwa mgan
ga huyo kwa miaka miwili bila kurudi nyumbani.
Alidai wiki mbili zilizopita, aliamua kuondoka kwa mganga huyo kwa miguu akiwa amefuga ‘rasta’ na kuvaa kaniki na ngozi, masharti ambayo alipewa na mganga wake ili tatizo lake liweze kumalizika.
Alisema akiwa njiani kurudi nyumbani, alifika katika kijiji cha Mwalubungwe, na kwenda nyumba ya mkazi wa kijiji hicho kuomba chakula kutokana na njaa.
“Alipofika katika nyumba hiyo alikuta watoto wanacheza nje.Kwa mwonekano aliokuwa nao, walimpiga kwa mawe na kumwita mwizi, kisha mzazi mmoja akapigana naye huku akipiga kelele, watu walifika na kumshambulia na hatimaye alipoteza maisha na kumzika bila nguo wala sanda,“ alisema Kamera.
Alisema taarifa za kifo cha mwanawe, alizipata kwa mtu aliyemwambia kuna mtu ameuawa ambaye alijitambulisha kwa jina la Kamera.
Alifuatilia na kufukua kaburi hilo na kukuta ni mwanawe. Alichukua maiti na kumzika tena.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alipohojiwa kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa. Lakini, aliahidi kufuatilia ili kufahamu undani wake.
CHANZO HABARILEO.
Post a Comment