Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa kozi ya Uofisa na
Ukaguzi wa Jeshi la Polisi leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi,
Kurasini, Jijini Dar Es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhitimu wa Kozi ya
Ukaguzi wa Polisi INSP. Leah Cheyeki kwa niaba ya Wahitimu wenzake
kutokana na kufanya vizuri katika Mafunzo hayo. Sherehe za kuhitimisha
Mafunzo hayo zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi leo Kurasini,
Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo pichani.
Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika leo katika Chuo cha
Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Kikosi
cha Judo kikionesha Onesho Maalum la namna ya kupambana na Mhalifu
ambaye hataki kutii amri halali ya Polisi. Sherehe za kufunga Mafunzo ya
Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi zimefanyika Chuo cha Taaluma ya
Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(wa pili
kutoka kushoto mwenye suit nyeusi)akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama ambao wamehudhuria Sherehe hizo za ufungaji Mafunzo ya Kozi ya
Uofisa na Ukaguzi wa Polisi(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Baadhi
ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za Ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa
na Ukaguzi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini
Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Post a Comment