Meneja
Uendeshaji wa Kampuni ya Udalali ya Flamingo, Nyalila Noel akipandika hati ya
mahakama katika basi la Shirikisho la soka Tanzania (TFF), ambayo inaruhusu
kukamatwa kwa mali za shirikisho hilo.
Meneja
Uendeshaji wa Kampuni ya Udalali ya Flamingo, Nyalila Noel akibandika hati ya
mahakama katika basi la Shirikisho la soka Tanzania (TFF), ambayo inaruhusu
kukamatwa kwa mali za shirikisho hilo.
Dereva la
basi dogo la TFF (kulia), akisoma hati ya mahakama iliyotolewa kwa ajili ya
kukamatwa kwa mali za TFF kutokana na deni la sh. milioni 51 linazodaiwa na
Safina Holding.
'Sasa
tunafunga na kuondoka nalo'.
Wafanyakazi
wa Jay Ambe Break Dowan wakichakalika na ufungaji wa basi la TFF tayari kwa
ajili ya kuondoka nalo kutokana na deni wanalodaiwa na Safina
Holding.
Gari dogo
aina ya Toyota Crown lenye namba T 643
BJW likiwa limezuia gari la Jay Ambe
Break Down lisitoke katika lango kuu la kutoka na kuingia katika Ofisi za TFF,
baada ya mali za shirikisho hilo kukamatwa na dalali wa
mahakama.
Hati ya
kukamata mali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikiwa imebandikwa katika
basi kubwa aina ya Youtong kwa ajili ya utekelezaji
Katibu Mkuu
wa TFF, Angetile Osiah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sakata
hilo.
Na
Mwandishi Wetu
UONGOZI wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo umejikuta kwenye wakati mgumu baada ya
madalali wa Kampuni ya Flamingo Auction Mart, kutinga katika ofisi za shirikisho
hilo na kukamata baadhi ya mali zake ili zipigwe mnada kufidia deni
wanalodaiwa.
Shirikisho
hilo linadaiwa na Safina Holding ya jijini Dar es Salaam zaidi ya sh milioni 50,
baada ya kuwaweka katika hoteli ya kampuni hiyo maeneo ya Kijitonyama, waamuzi
wa michuano ya Kombe la Kagame mwaka 2012.
Sakata hilo
liliweza kudumu kwa muda wa saa nne kuanzia saa tano asubuhi na kudumu hadi saa
tisa mchana, baada ya TFF kukubali kulipa sh milioni 20 kati ya sh 51,507,012
zilizokuwa zikidaiwa.
Awali,
madalali hao wa Flamingo, walifika Ofisi za TFF, Karume Ilala na kujadiliana na
Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah na kushindwa kufikia muafaka,
hali iliyowalazimu kuita gari maalumu ‘break down’ mali ya Jay Ambe na kulifunga
basi dogo aina ya Toyota Coaster.
Baada ya
gari hilo kufungwa ili likokotwe kupelekwa ‘yadi’ ya Flamingo, mlinzi wa TFF
aliamua kukimbilia geti la kutokea na kulifunga na kuwafanya madalali hao
washindwe kutoka nalo.
Jambo hilo
lilizidisha sintofahamu na kuwafanya baadhi ya watu kuingia ndani kushuhudia
kinachoendelea, huku maofisa wa Flamingo wakihangaika kuwasiliana na Jeshi la
Polisi kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuweza kutekeleza amri ya
mahakama.
Usumbufu
huo wa kuzuia madalali wasitekeleze amri halali ya mahakama, ulisababisha kero
kwa watu mbalimbali waliofika Karume, kwa kushindwa kuingia ama kutoka katika
ofisi hizo.
Wakati
majadiliano yakiendelea, zilipatikana taarifa kuwa TFF wameomba walipe sehemu ya
fedha wanazodaiwa kwa ahadi ya kumalizia zilizobaki, ili magari yake
yasichukuliwe, hali iliyomfanya dereva wa gari lililozuia mlango kwenda
kuliondoa na kuruhusu shughuli zingine kuendelea.
Ilipofika
saa tisa mchana, Osiah alijitokeza na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa
wamemuagiza mhasibu akachukue fedha benki.
Akizungumzia
adha hiyo, Osiah alisema wao hawakujua kama tukio hilo litatokea, kwa kuwa barua
waliyokuwa nayo haikueleza hivyo, na kudai kushangazwa na hatua hiyo, wakati
barua kutoka Flamingo ikionekana kuchanganya tarehe ya zoezi hilo
kufanyika.
Osiah
alisema walipata nguvu za kugoma magari hayo yasichukuliwe kutokana na kugundua
kuna makosa ya tarehe katika barua hiyo, huku akikiri kudaiwa sh milioni
28.
“Sisi
tunadaiwa mil 28/-, ila mambo ya kimahakama ndio maana ikafikia hiyo na pia
tumewashangaa sana Safina, badala ya mambo tuyamalize wenyewe, wao wanayakuza na
fedha hizo zilitokana na hifadhi ya waamuzi katika michuano ya Chalenji,”
alisema Osiah.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Flamingo, Deogratius Luziga, alisema wao walifikia hatua
hiyo ya kutaka kuondoka na magari hayo kama amri ya mahakama ilivyowaagiza na
kudai kuwa tatizo kubwa ilikuwa ni dharau za Osiah na kuwa angefanya hivyo toka
awali wasingechukua muda wote huo katika zoezi hilo.
“Tumekubaliana
mara baada ya kutuomba sana, tumekubali watangulize milioni 20/- kwanza, halafu
milioni 31/- watamaliza ndani ya siku 14, kwani hii mahakama inaruhusu na bila
hivyo, tutafanya kama tulivyokusudia kwa kuwa bado ni mali yetu sisi,” alisema
Luziga.
Awali,
Osiah alionekana kuchanganyikiwa na kuwasihi madalali hao kuachana na zoezi hilo
la kuchukua magari hayo.
“Naombeni
muache kufanya hivyo ambavyo mnataka kufanya, mimi sasa hivi namwambia mhasibu
wetu mwende naye benki akawape fedha zenu zote jamani, msifanye hivi,” alisihi
Osiah.
Post a Comment