Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robert
Kazinza akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Shinyanga Hawapo pichani walio jitokeza
kushuhudia fainali za Mashindano ya Ngoma za ASili kwa mkoa huo chini ya
udhamini wa kampuni hiyo kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Mkuu wa
wilaya Ya Shinyanga Anna Rose Nyamubi na anaye fuatia aliye vaa mawani ni Afisa
Utamaduni Manispaa Asha Mbwana wakimsikiliza kwa makini Meneja
huyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Anna Rose Nyamubi
akikabidhi zawadi ya mshindi wa pili wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili
mkoa wa Shinyanga fedha tasilimu shilingi laki tano kwa kiongozi wa kundi la
Mabulo ya Jeshi Nkuba shija , kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni ya bia
Tanzania(TBL) mkoa wa Shinyanga Robert Kazinza na wanne kutoka kushoto ni Meneja
matukio wa Kampuni hiyo Erick Mwayela Mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni
ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Anna Rose
Nyamubi(kushoto) akikabidhi zawadi kiongozi wa kundi la Ngoma la Mabulo ya
Jeshi shilingi laki tano mara baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano
ya Balimi Ngoma Mkoa wa Shinyanga yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Kushoto ni
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Shinyanga, Robert Kazinza
na Meneja matukio TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela.
Mshehereshaji katika fainali za mashindano ya ngoma za
asili kwa Mkoa wa Shinyanga kutoka Kampuni ya Integrated Communication Kabwera
akiwa na kiongozi wa kundi la Mwanajilunguja Ngelela Ng'wanajilunguja kwa pamoja
wakiimba nyimbo ya kuipongeza Bia ya Balimi Extra kwa kudhamini shindano hilo
kabra ya kukabidhiwa fedha tasilimu shilingi laki sita ikiwa kama zawadi ya
mshindi wa kwanza na mkuu wa wilaya Anna Rose Nyamubi ambaye anaonekana kwa
nyuma amezishikilia fedha hizo.
Kiongozi wa kundi laNgoma la Wagoyangi, Ngelela
Ng'wanajiluguja(katikati) akifurahia kitita cha shilingi laki sita mara baada ya
kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Annarose Nyamubi(wa pili kushoto)
mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinyanga
yanayodhaminiwa na Bia ya Balimi,yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani
humo.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Shinyanga,
Robert Kazinza na Meneja matukio TBL Kanda ya Ziwa, Erick
Mwayela.
Wasanii wa kundi la ngoma za asili la Mabulo ya Jeshi
ambao wameshika nafasi ya pili katika fainali za Mashindano ya ngoma za asili
wakitumbuiza mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo ambalo limefanyika
katika viwanja vya Shaykomu mjini hapo Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni
ya Bia Tanzani kupitia bia yake ya Balimi Extra.
KUNDI la Ngoma la Mwanajilunguja limefanikiwa kutwaa
ubingwa wa mashindano ya Ngoma Mkoa wa Shinyanga yanayodhamniwa na Kampuni ya
Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra Lager yaliyomalizika
mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Kundi la Mwanajilunguja lilitwaa ubingwa huo kwa alama
82,na kuzawadiwa fedha taslimu Sh.600,000/= na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa
Shinyanga katika fainali za mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika Julai
20 mwaka huu jijini Mwanza.
Washindi wa pili katika mashindano hayo ni kundi la
Mabulo ya Jeshi ambao walipata alama 80 hivyo kujinyakulia fedha taslimu
Sh.500,000/=,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kundi la Wagoyangi Usule kwa alama
79 na kuzawadiwa Sh.400,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na Wagoyangi Bugimbagu
kwa alama 73 ambao walizawadiwa Sh.400,000/=
Jumla ya vikundi vilivyoshiriki mashindano ya Ngoma
Mkoa wa Shinganga ni 10,ambapo vikundi shiriki 6,vingine vilipewa kifuta jasho
cha fedha taslimu Sh.150,000/= kila kikundi.
Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo pamoja na
wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, Mkuu wa Wilaya ,Anna
Rose Nyamubi aliwapongeza washiriki wote kwa ushiriki wao katika mashindano hayo
na pia kwa kuendeleza mila na desturi za ngoma za asili lakini zaidi aliipongeza
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Balimi Extra Lager ambao wanadhamini
mashindano hayo kwa kujua udhamani wa Ngoma za asili.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa kwa kutumia mashindano
kama hayo jamii imekuwa ikiburudika kupitia tamaduni zetu ambazo mara nyingi
zimekuwa zikisahaulika kwa wengi na kuiomba kampuni ya TBL kuendelea kudhamini
mashindano hayo na kuwataka kutosita kushilikiana na serikali katika masuala
mbalimbali ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia baadhi ya
majukumu ya serikali.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amevitaka vikundi hivyo
kuzitumia fedha wanazo zipata katika kujiletea maendeleo ikiwemo kuanzianzisha
vikundi vya kuweka na kukopa ili viweze kuwasaidia katika kuwalete
maendeleo.
Naye Meneja wa Kampuni ya bia Tanzani (TBL) Robert
Kazinza amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa
jamii kwa kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze
kuendelea kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao, hasa
bia ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa pekee.
Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki katika fainali hizo
ni pamoja na Buzoli Ngunga, Kadete, Wagoyangi Maswa, Waulinguli Bugimbagu,
Bugali na Shinyanga Art Group, fainali hizo zitaendelea wiki ijayo ili kumpata
mshindi wa fainali hizo katika mkoa wa Kagera, ambaye ataungana na washindi
wengine ambao watashiriki mashindano hayo ngazi ya kanda yatakayo fanyika jijini
Mwanza Hivi karibuni.
VIA/http:ipshamedia.blogspot.com
Post a Comment