Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI , CCM YAIZIKA RASMI CHADEMA IRINGA



CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeshinda kwa kimbunga uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Mbalamaziwa wilaya ya Mufindi na kata ya Nga'ang'ange wilaya ya Kilolo mkoani Iringa dhidi ya chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)

Katika matokeo hayo ya uchaguzi ambayo mtandao huu wa www.matukiodaima.com umeyapata kwenye kata ya Ng'ang'ange wilaya ya Kilolo ambayo msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo Esabela Kamwela ameyatangaza amesema kuwa jumla ya wapiga kura walikuwa 919 kati ya 1087 waliojiandikisha kupiga kura.

Alisema kuwa katika uchaguzi huo ambao umemalizika katika hali ya utulivu na amani mgombea wa Chadema alikuwa ni Lucas Chaye na mgombea wa CCM alikuwa ni Namgeleki Yohanas na kuwa wagombea wote wamekubali matokeo na kusaini fomu za uchaguzi za tume .

Kamwela amesema kuwa katika uchaguzi huo jumla ya kura 16 ndizo zilizoharibika na kura 903 zilipigwa huku mgombea wa Chadema akianguka vibaya kwa kupata kura 217 na mgombea wa CCM akiimbuka kidedea kwa kura 686.

Wakati kagtika kata ya Mbalamaziwa ambako pia kulikuwa na mvutano mkubwa wa uchaguzi kati ya CCM na Chadema kiasi cha wafuasi wake kutambiana kwa kupigana nguvu wakati wa kufunga kampeni pia Chadema imepata pigo kubwa baada ya kushindwa vibaya dhidi ya CCM.

Mbalamaziwa ambako ni jirani kabisa na kata ya Nyololo ambayo mwaka jana mwezi wa tisa mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi aliuwawa katika vurugu za Chadema na polisi pia Chadema imeonekana kukataliwa na wananchi baada ya mgombea wake Ezekiel Mlyuka kuambulia kura 185 pekee huku mgombea wa CC Zuberi Nyomolelo akizoa kura 1426 na kura 26 zikiharibika .

Hata hivyo matokeo hayo yamepokelewa kwa mikono miwili toka kwa wagombea wote na sasa inasubiriwa siku ya kuapishwa kwa madiwani hao wateule.
Download Our App

1 comments:

kwa kweli mimi ninaona hawa CHADEMA nao hawawezi biashara ya jumala jumla wala ya leja leja.bora wabadilishe fbiashara labda ya kuuza bloila

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top