MBUNGE wa Kondoa Kaskazini Zabein Mhita (pichani), jana alitoa machozi bungeni
alipokjuwa akielezea matatizo makubwa yanayowapata wananchi wa jimbo
lake kwa kukosekana mawasiliano ya simu. Alikuwa akishiriki kwenye
mjadala wa makadirio ya matumizi na matumizi ya Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia. Mhita alifikia wakati akatoa machozi baada ya
kueleza kuwa alipata taarifa za kifo cha mtoto wake mwaka 2005 akiwa juu
ya mti.
Wakati huo alikuwa Naibu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia.
“Nilipata taarifa za kifo cha mtoto wangu nikiwa juu nya mti. Kwa kweli hii inahuzunisha sana.
“Wananchi wa Kondoa Kaskazini wafanye nini ili waeleweke jinsi wanavyoteseka kutokana na kukosekana mawasiliano,” alisema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.
Alisema katika jimbo hilo ni vigumu kupata mawasiliano hadi mtu apande kwenye jabali au mti.
Baada ya kumaliza kutoa mchango wake huku akiendelea kujifuta machozi baadhi ya wabunge wenzake wanawake walikwenda kumfariji na kumpa pole.
Baadaye akichangia hotuba hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alionyesha kuhuzunisha na yaliyoendelea kuwapata wananchi wa Kondoa Kaskazini na hasa lililompata Mhita.
Alisema serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha tatizo la mawasiliano linapungua au linaondolewa Kondoa Kaskazini, ingawa alisema serikali haina uwezo wa kujenga minara ya simu.
Kuhusu Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) alisema matatizo makubwa yaliyokuwa yanaikabili yamekwisha kushughulikiwa.
Matatizo hayo ni menejimenti mbovu, wizi na mtaji mdogo.
Alisema baadhi ya watumishi wabadhirifu waliokuwa kwenye menejimenti wamekwisha kusimamishwa kazi na mazungumzo yanaendelea na Kampuni ya Airtel ili serikali iweze kununua hisa za asilimia 35 za kampuni hiyo katika TTCL.
Mazungumzo hayo yatakuwa yamefikia mwisho kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambako serikali itaweza kuimiliki TTCL kwa asilimia 100.

Post a Comment