SERIKALI inapoteza Sh bilioni 15, kutokana na kuingizwa nchini kwa
saruji ya magendo ambayo hailipiwi ushuru wala kodi nyingine, jambo
lichangialo upotevu wa mapato. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Saruji Tanzania (TCCL), Erik Westerberg katika hafla ya
makabidhiano ya nyumba tatu za polisi zilizoko Makorora, ambazo
zimekarabatiwa na kampuni hiyo.
Alisema ipo saruji nyingi ya magendo ambayo inaingizwa nchini kinyemela na kuuzwa kwa bei ya chini kuliko inayozalishwa na viwanda vya ndani, hali inayosababisha kushuka kwa mauzo ya viwanda vya nchini.
Alisema iwapo Serikali hatachukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa viwanda vya ndani kufa au kuzalisha bidhaa chini ya kiwango, ili waendane na soko.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alisema kukamilika kwa ukarabati wa nyumba hizo ni faraja kwa jeshi kwani zitapunguza tatizo la askari kuishi mbali na maeneo ya kazi na hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji.
“Natoa wito kwa wadau wengine, kuunga mkono juhudi za Tanga Cement kutuunga mkono jeshi la polisi katika harakati zake za kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuwatengenezea mazingira bora ya kazi,” alisema Massawe.
Kampuni ya Saruji ya mkoani hapa, imetumia Sh milioni 26 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Polisi zilizoko katika eneo la Makorora.
Na Amina Omari, Tanga MTANZANIA

Post a Comment