Katibu
wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women Association,Viola
Lindikikok akitoa mada katika mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na
asasi hiyo na kuwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka katika kata za
lemara na Daraja mbili za jijini Arusha,pembeni yake ni wahamasishaji
katika mdahalo huo
Mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola akitoa semina yaelimu ya uraia iliyoandaliwa na taasisi ya Mategemeo Women Association ya jijini Arusha
……………………………………………………………..
Imeelezwa
ya kwamba vijana wengi nchini hawana uelewa wa elimu ya uraia hali
ambayo imepelekea baadhi yao kushindwa kutambua majukumu yao ya msingi
na fursa mbalimbali za kuwaingiza kipato.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women Association,Viola Likindikok wakati alipokuwa akizungumza katika mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo .
Mdahalo
huo uliwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka kata za Lemara na Daraja
mbili ambapo miongoni mwao ni wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo
ndani ya kata hizo.
Katibu
huyo alisema kwamba katika utafiti wao wamebaini ya kwamba vijana wengi
nchini hawana elimu ya kutosha kuhusu suala la uraia hali ambayo
imekuwa ikichangia kushindwa kujitambua.
Hatahivyo,alisisitiza ya kuwa katika
midahalo mbalimbali waliyoifanya vijana wengi wamekuwa wakihoji kuhusu
suala la ajira ambalo alikiri ni changamoto kuu kwa serikali na kila
mdau wa maendeleo hapa nchini.
Naye,mkuu
wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola alisema ni vyema
vijana nchini wakapewa elimu ya uraia ili waweze kujitambua na kuepuka
kutumiwa katika harakati mbalimbali za kichochezi.
Baadhi
ya watoa mada katika mkutano huo,Happy Mwajunga na Salmin Sulle
walisema kuwa waliwataka vijana kuacha kulalamika na kukata tamaa katika
maisha huku wakiwasisitiza kuwa wadadisi ili waweze kutambua fursa
mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Post a Comment