Dk. Mervyn MansellMmoja wa wahanga wake
Moses Sithole
Mnamo Septemba 17,
1995, Dk. Mervyn Mansell aliombwa na Polisi ili kusaidia kujua tarehe ya kifo
cha mwili wa mtu uliyookotwa katika pori lililoko katika eneo la machimbo ya
madini la Van Dyke eneo ambalo lipo jirani na mji wa Boksburg nchini Afrika ya
kusini. Dk. Mansell mtaalamu wa elimu ya wadudu akifanya kazi katika kitengo cha
utafiti wa kilimo katika halimashauri ya jiji la Pretoria alikuwa amepata
taarifa hizo wiki mbili mapema kutoka kwa askari wa upelelezi aitwae Vivian
Bieldt.
Askari huyo alikuwa amesoma utafiti fulani kuhusiana na funza kutumika kukadiria siku kifo kilipotokea kwa usahihi kabisa pale inapotokea mwili wa mtu aliyeuawa na kutekelezwa mahali na kuonekana baada ya siku kadhaa ukiwa umeshaanza kuharibika kwa kushambuliwa na funza.
Askari huyo alikuwa amesoma utafiti fulani kuhusiana na funza kutumika kukadiria siku kifo kilipotokea kwa usahihi kabisa pale inapotokea mwili wa mtu aliyeuawa na kutekelezwa mahali na kuonekana baada ya siku kadhaa ukiwa umeshaanza kuharibika kwa kushambuliwa na funza.
Siku hiyo hiyo baadae Inspekta Bieldt alimpigia tena
simu Dk. Mansell na kumjulisha kwamba, sio mwili wa mtu mmoja tena bali
wamegundua miili ya watu watano. Kwa upande wa Dk. Mansell hii ilikuwa ni kesi
ya kwanza nchini humo kuwahusisha wataalamu wa elimu ya wadudu katika upelelezi.
Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba mpaka siku ya pili wakiendelea kufanya
upelelezi katika eneo hilo, walipata jumla ya miili watu kumi wote wakiwa ni
wanawake. Hiyo ilionyesha kwamba muuaji alikuwa akiuwa na kufika pale kuitelekza
miili ya watu aliowauwa katika eneo hilo.
Mwili wa kwanza uligunduliwa siku ya Jumamosi jioni
ya Septemba 16 1995, wakati Polisi mmoja alipotoka na mbwa wake kwenda kuwinda
sungura katika pori hilo. Zaidi ya Polisi 30 wakiwemo askari wa upelelezi kutoka
katika kitengo cha upelelezi wa kesi za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha
cha East Rand waliwasili katika eneo hilo, pia walikuwepo wataalamu wa kukusanya
ushahidi kitaalamu ambao walikuwa na jukumu kubwa la kuchunguza eneo la tukio
ili kukusanya ushahidi kwa siku kadhaa.
Si hivyo tu, bali pia Helikopta na mbwa wa Polisi
vilihusishwa ili kuchunguza iwapo kulikuwa na miili mingine iliyotelekezwa
katika eneo hilo.Micki Pistorius Polisi na mwanasaikolojia alikuwepo pia katika
eneo hilo. Akizungumzia hali aliyokutana nayo katika eneo hilo, alisema kwamba
hali ilikuwa ni ya kutisha sana na hajawahi kukutana na hali hiyo tangu kuzaliwa
kwake.
“Haya ni moja ya mauaji ya kutisha ambayo
sijapata kuyashuhudia katika maisha yangu, miili ya watu waliouawa ilikuwa
imetapakaa kila mahali huku mingine ikiwa imekaribiana kwa umbali wa mita kadhaa
kutoka ulipo mwili mwingine. Funza walikuwa ni wengi katika eneo hilo kiasi cha
kutupanda katika nguo zetu.” Alisema mama huyo, Polisi na
mwanasaikolojia.
Kuna uwezekano kwamba baadhi ya wanawake wale
waliouawa katika eneo hilo na kutelekezwa mahali hapo. Ilikuwa ni vigumu kuamini
kwamba muuaji alikuwa akiwachukua wahanga wake na kuwapeleka katika eneo hilo
ambapo kulikuwa na miili ya watu waliuawa na muuaji huyo tena ikiwa tayari
imeshaanza kuharibika ili kuwatisha na kuwajengea hofu kabla ya kuwabaka kuwauwa
na kutelekeza miili yao mahali hapo.
Ili kuthibitisha kuwa lengo la muuaji kuwapeleka
wahanga wake katika eneo hilo ni ili kuwatisha na kuwajengea hofu, mmoja wa
wanawake waliouawa alikuwa amejikojolea kwenye suruali yake ya jinzi kwa hofu
kabla ya kuuawa.Wakati Polisi wakiendelea kujitetea kutokana na mauaji ya
Mtuhumiwa wa mauaji ya kutisha David Selepe aliyeuawa Desemba 17, 1994 akiwa
mikononi mwa Polisi, walidai kwamba wana ushahidi ambao unamuhusisha David
Selepe na vifo vya wanawake sita ambao miili yao ilipatikana katika eneo la
Cleveland.
David Selepea alikuwa akituhumiwa kwa vifo vya
wanawake 4, lakini alipokamatwa alikiri kuuwa wanawake 15. Ni wakati alipokuwa
akiwapeleka askari wa upelelezi katika eneo alipotekeleza miili ya wanawake
wengine ndipo alipouawa kwa kupigwa risasi ya kichwa wakati alipojaribu
kutoroka. Polisi waliamini kwamba yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya vifo vya
wanawake hao sita.
Mwili wa kwanza ulipatikana hapo mnamo Januari 4,
1995, ukiwa umetelekezwa porini nusu uchi. Mwili wa mwanamke huyo haukupata
kutambuliwa. Mwili wa pili ulipatikana hapo mnamo Februari 9. Alikuwa ni
mwanamke na alikuwa uchi wa mnyama na nguo zake ziliwekwa kifuani mwake zikiwa
zimewekewa jiwe juu yake.
Alama zake za vidole ndizo zilizoharakisha
kutambuliwa kwake. Alikuwa ni binti mrembo aliyejulikana kwa jina la Nuku Soko
aliyekuwa na umri wa miaka 27. Alipotea tangu Januari pale alipoaga kwamba
anakwenda kwa dada yake aishie katika eneo la Klipgat, na hakuonekana tangu siku
hiyo.
Asubuhi ya Machi 6, wafanyakazi wa ujenzi walikuwa
wanachimba shimo katika eneo la Atteridgevile, na walipatwa na mshtuko walipoona
matiti ya mwanamke kuashiria kwamba kulikuwa na mwili wa mwanamke uliozikwa
katika eneo hilo. Waliufukua mwili huo na baadae ulitambuliwa kwamba ni wa
mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Sara Matlakala
Mokono.
Alikuwa na umri wa miaka 25, na lipotea siku tatu
zilizopita wakati akiwa njiani kwenda kuonana na mtu aliyemuahidi kumpatia
kazi.Mnamo April 12 mwili mwingine uligunduliwa katika eneo la Atteridgeville.
Mwanamke huyo mikono yake imefungwa kwa nyuma kwa kutumia sidilia yake. Alikuwa
amenyongwa. Ingawa nguo zake zilikuja kuonekana katika eneo hilo lakini chupi
yake haikupata kuonekana.
Alikuja kutambuliwa baadae kama Letta Nomthandazo
Ndlangamandia aliyekuwa na umri wa miaka 25.
Mnamo April 17, gazeti
maarufu nchini humo linaloandikwa kwa lugha ya Afikaans liliibuka na habari
kwamba kuna miili ya wanawake wanne imegunduliwa na likahitimisha kwa kusema
kwamba mtindo uliotumika katika kutekeleza mauaji hayo (modus operandi)
unafanana kabisa na namna muuaji maarufu wa Cleveland alivyokuwa akiuwa ambaye
anaaminika kuwa ni Davidi Selepe.
Mnamo April 19, Polisi walitangaza rasmi kwamba kuna
uwezekano kuna muuaji mwingine anayeendesha mauaji kaika eneo hilo la
Atteridgeville. Walituhumu kwamba huenda kuna mtu anaiga mtindo wa muuaji wa
Cleveland ili kuwachanganya askari wa upelelezi.
Siku iliyofuata mwili wa mtoto wa kiume uligunduliwa
jirani kabisa na ulipokutwa mwili wa Letta Ndlangamandla. Ilibainika kwamba
mwili huo ni wa mtoto aitwae Sibusiso aliyekuwa na umri wa miaka
2.
Mwili huo ulikutwa umbali wa futi 65 kutoka
ulipokuwa mwili wa mama yake. Letta aliondoka mapema Mwezi April kwenda
Mashariki mwa jiji la Pretoria kukutana na mtu ambaye alimuahidi kumpatia
kazi.
Kwa kuwa hakuwa na mtu wa kumuachia mwanaye Letta
aliamua kuondoka naye. Wataalamu wa uchunguzi wa maiti walishindwa kubaini
sababu ya kifo cha mtoto huyo ingawa alikuwa na jeraha kichwani na haikujulikana
ni yupi alitangulia kufa kati ya mama au mtoto.
Kulikuwa na uwezekano kuwa mtoto Sibusiso alikufa
kutokana na kupigwa na baridi kali porini baada ya mama yake
kuuawa.
Hebu fikiria mtoto mdogo wa miaka miwili alikuwa
akirandaranda porini peke yake karibu na ulipolala mwili wa mama yake kwa sababu
hakujua mahali pa kwenda kutokana na kuwa na umri mdogo hadi
alipokufa.
Mnamo may 13, mwili wa Esther Moshibudi Mainetjas
uligunduliwa katika msituni jirani na eneo la Hercules magharibi mwa jiji la
Pretoria.
Alikuwa nusu uchi na alikuwa amenyongwa kwa kutumia
nguo. Kwa mara ya mwisho alionekana jioni ya siku
iliyopita.
Mwili wa mwanamke mwingine uligunduliwa mwezi mmoja
baadae, ingawa kulikuwa na wanawake wengine watano waliotoweka katika mazingira
ya kutatanisha kwa nyakati tofauti.
Francina Nomsa Sithebe aliyekuwa na miaka 25, mwili
wake ulikutwa ukiwa umekalishwa ukiwa umeegemea mti hapo mnamo Juni 13. Ingawa
alikuwa amevaa gauni.
wachunguzi wa maiti walibaini kwamba chupi yake na
mkanda wa mkoba wake ulikuwa umefungwa shingoni mwake na kisha ukafungwa kwenye
mti.Siku tatu baadae, mnamo Juni 16, Elizabeth Granny Mathetsas mwili wake
uligunduliwa ukiwa uchi katika eneo la viwanda la Rosslyn kama maili 9 kaskazini
magharibi mwa jiji la Pretoria. Alikuwa na umri wa miaka 19 na mara ya mwisho
alionekana akiwa hai hapo mnamo Mei 25.
Mnamo Juni 22 mwili wa mwanamke mwingine
uligunduliwa katika eneo la Rosherville. Alikuwa amebakwa na kisha kunyongwa.
Nyaraka za utambulisho wake zilikutwa katika eneo hilo na kurahisisha
kutambuliwa kwake.
alikuwa anaitwa Ernestina Mohadi Mosebo. Alikuwa na
umri wa miaka 30.Siku mbili baadae mnamo Juni 24, mwili wa Nikiwe Dikos
uligunduliwa katika eneo la Atteridgeville.
Alikuwa ametoweka tangu April 7, wakati alipoaga
kuwa anakwenda kuonana na mtu aliyemuahidi kumpatia kazi. Mwili wake ulikuwa
umeshambuliwa na mbwa mwitu kiasi cha kutawanywa vipande vpande kila mahali.
Mikono yake ilikuwa imefungwa na chupi yake.
Kutokana na mwili wake kutawanywa na Mbwa Mwitu,
Polisi walifanikiwa kupata fuvu la kichwa chake siku iliyofuata, futi 130 kutoka
yalipolala mabaki ya mwili wake.
Alkuwa amenyongwa kwa kutumia chupi yake ikiwa
imekazwa kwa kutumia kipande cha mti, pia kulikuwa ana kipande cha mti
kilichosokomezwa kwenye uke wake. Alikuwa amevaa pete yake ya ndoa na mabaki ya
mwili huyo yalitambuliwa na mumewe.
Absolom Sangweni alikuwa akiishi kwenye nyumba yake
ya turubai katika eneo la Beyers Park katika mji wa Boksburg. Mnamo July 17,
1995, aliwaona mwanaume na mwanamke wakitmbea kuelekea kwenye kijipori
kilichokuwa jirani na hapo nyumbani kwake. Kwa kuwa alikuwa anajua kwamba kuna
uzio uliozungushwa katika kijipori hicho alijua watu wale wasingeweza kuendelea
na safari yao.
Aliwaita, lakini yule mwanaume alimjibu kwamba
analifahamu vizuri eneo hilo. baadae kidogo walipotea machoni mwake. Hata hivyo
Absolom aliendelea kuchunguza walipopotelea watu wale.
Baadae kidogo alimuona yule mwanaume akitokea lakini
akiwa peke yake. Absolom alidai kuona kitu kinachong’aa mkononi mwa mwanaume
yule na alikuwa akiangalia huku na huko kama vile alikuwa na wasiwasi kwamba
kuna mtu amemuona akifanya jambo na hivyo alikuwa anataka kuondoka katika eneo
hilo haraka iwezekanavyo. Hata hivyo alitoweka.
Absolom alikwenda katika kijipori hicho na kumkuta
yule mwanamke akiwa amenyanyaswa kijinsia na alikuwa amepoteza fahamu. Absolom
alikwenda katika supermarket moja iliyokuwa jirani na kuwajulisha Polisi
waliokuwa katika eneo hilo. Sajenti Gideon ONeal alifika katika eneo la tukio na
kumkuta mwanamke huyo akiwa amepoteza fahamu. Hakukuta mkoba wa mwanamke huyo na
hivyo kupata ugumu wa kumtambua.
Askari mwenzake aliwasili katika eneo hilo akiwa na
mkoba wa huduma ya kwanza lakini walishindwa kuokoa maisha yake. Alifariki
dunia. Alikuwa amenyongwa na mkanda wa gauni lake. Absolom alidai kwamba alikuwa
mbali na hakuweza kumtambua mwanaume huyo.Mwanamke huyo altambuliwa kwa jina la
Josephine Mantsali Mlangeni. Alikuwa na mri wa miaka 25 na mama wa watoto
wanne.
Alikuwa ameaga nyumbani kwamba anakwenda kukutana na
mtu ambaye alimwahidi kumapatia kazi nzuri.Miili mingine ya wanawake waliouawa
iliogunduliwa ni hii ifuaayo:
Granny Dimakatso Ramela. Mwili wake uligunduliwa
Magharibi mwa jiji la Pretoria. Alikuwa akiwa amelala kifudifudina kamba
iliyotumika kumnyongea ilikuwa bado iko shingoni mwake. Alikuwa na umri wa miaka
21 na alikuwa ametoweka kusikojulikana tangu Mei 23.
Mildred Ntiya Leple aliyekuwa na umri wa miaka 28
alipelekwa Pretoria na mumewe baada ya Granny Ramela kutoweka, ili kuonana na
mtu ambaye alimwahidi kumpatia kazi.
Hakupata kumuona mke wake tena hadi pale mwili wake
ulipopatikana hapo mnamo Julai 26 jirani na bwawa la Bon Accord karibu na mji wa
Onderstepoort, takriban maili 9 kaskazini mwa jiji la Pritoria. Alikuwa
amenyongwa kwa kutumia chupi yake.
Polisi ilibidi waandae chumba maalum cha kufanyia
uchunguzi wa miili ya wanawake iliyokuwa ikiokotwa kila uchao baada ya kuuawa
kwa mtindo unaofanana.Mnamo August 8, mwili mwingine wa mwanamke uligunduliwa
katika mji wa Onderstepoort.
Alitambuliwa kutokana na nyaraka zilizokutwa ndani
ya mkoba wake. Alijulikana kwa jina la Elsie Khoti Masango aliyekuwa na umri wa
miaka 25. Alikuwa ametoweka tangu Julai 14.
Mwili wa mwanamke mwingine uligunduliwa katika eneo
hilo hilo, lakini ulikuwa umechomwa moto kiasi cha kutotambuliwa. Haikujulikana
kwamba mwili ule ulikuwa umetelekezwa katika eneo hilo kwa muda
gani.
Wiki mbili baadae mnamo Agost 23, mwili wa mwanamke
mwingine aliyejulikana kwa jina la Oscarina Vuyokazi Jakalases aliyekuwa na umri
wa miaka 30 uligunduliwa jirani na eneo la Boksburg. Alikuwa ametoweka siku
ulipopatikana mwili wa Elsie Masangos. Ilikuwa ni Agosti
8.
Mnamo Agosti 28 na 30, miili mingine ya wanawake
wawili iligunduliwa katika bwawa la Bon Accord karibu na mji wa
Onderstepoort.
Mwili wa mwanamke wa pili ulionyesha kwamba
ulitelekezwa kwa miezi kadhaa katika eneo hilo, na haukuweza kutambuliwa.Kwa kifupi ni kwamba kwa nyakati tofauti miili zaidi ya
wanawake 38 ilipatikana katika maeneo tofauti tofauti wote wakiwa wameuawa kwa
mtindo unaofanana huku wengine wakiwa wamebakwa.
Kutokana na
mauaji hayo ya kutisha na ya mfuatano, yaliwapa askari wa upelelezi nchini humo
wakati mgumu, hivyo waliamua kuwatafuta wataalamu waliobobea kwa kazi ya
upelelezi nje a nchi hiyo hususan Ulaya au Marekani.
Mmoja wa wapelelezi wa kesi hiyo mwanamama Micki
Pistorius alikwenda kuhudhuria kongamano moja nchini Skotland mnamo Juni, ambapo
alikutana na Robert Ressler na Roy Hazelwood wote waliwahi kufanya kazi katika
shirika la upelelezi la Marekani FBI, lakini walikuwa wamestaafu wakati
huo.
baada ya kuzungumza nao walikubali kwenda nchini
humo kusaidia katika upelelezi wa kesi hiyo.Micki Pistorius akishirikiana na
Robert Rissler walitengeneza taarifa fupi kuhusiana na mauaji huyo ili
kurahisisha upelelezi wa kesi hiyo.
Taarifa hiyo ilionyesha kwamba kulikuwa na maeneo
maalum ambapo miili ya wanawake hao iliteekezwa. Wanawake nane waliouawa
walitupwa jirani na mji wa Atteridgeville akiwepo mtoto wa kiume wa miaka
miwili.
Miili ya wanawake sita iligunduliwa katika eneo la
Onderstepoort, miili ya wanawake wengine 12 ilikutwa imetupwa katika eneo la
Boksburg, pia kulikuwa na mwanamke aliyeokotwa jirani na mji wa Cleveland.
Wataalamu hao walibaini kwamba mauaji ya wanawake 27 yalikuwa
yanafanana.
Lakini pia waliamini kwamba huenda mauaji hayo
yalitekelezwa na muuaji zaidi ya mmoja. Ilionyesha kwamba maeneo ilipotelekezwa
miili hiyo ilikuwa imechaguliwa kwa umakini wa hali ya juu mno, na muuaji
(wauaji) alikuwa anawafahamu wahanga hao.
Maeneo ilipotupwa miili hiyo ilikuwa inafikika
kiurahisi na hata namna miili hiyo ilivyokuwa ikitelekezwa muuaji hakuonekana
kama alikuwaana dhamira ya kuificha ili isipatikane.
Miili mingine ilikuwa imelaliana.Katika taarifa yao
wataalamu hao pia walibainisha kwamba, wanawake wote waliouawa kwa mujibu wa
ndugu zao walikuwa wanaaga kwamba wanakwenda kuonana na mtu aliyewaahidi
kuwapatia kazi. Alikuwa anawabaka na kuwauwa na kisha kutelekeza miili
hiyo.
Walimuelezea muuaji huyo kama ni (1)mwanaume mweusi
mwenye umri kati ya mika 20 au alikuwa anakaribia miaka 30 (2)Alikuwa amejiajiri
ambapo likuwa ana uwezo wa kuwa na fedha za kutosha. (3) huenda alikuwa
anaendesha gari la kifahari. (4)anavaa mavazi ya gharama na vito vya thamani.
(5) ni mtu anayejichanganya na watu, mcheshi na ni mtu wa wanawake. (6) kuna
uwezekani ameoa, au ametengana na mke wake au ameachana na mke
wake.
(7) ni mtu wa kujirusha kwenye vilabu na
kujichanganya na watu. (8) anaweza kuwa anajihusisha na utapeli au wizi (9)
atakuwa anawafuatilia ripoti za Polisi jinsi wanavyofanya pelelezi wao kupitia
vyombo vya habari.
(10) anaonekana kuwa na chuki na wanawake ingawa
anaonekana kuwachangamkia.
(11) huwa anapiga punyeto baada ya kufanya mauaji
juu ya miili ya wanawake hao kabla ya kuitelekeza (12) anaonekana kupenda sana
wanawake na huwa anaangalia picha za ngono (13) kunauwezekano aliwahi
kunyanyaswa kijinsia alipokuwa jela hususan jela ya
watoto.
(14) anaonekana kuwa na akili sana na ni kijana wa
mtaani aliyebobea kwenye vitendo vya kihalifu.Mkoba wa mmoja wa wanawake
waliouawa na kutelekezwa katika eneo la Boksburg ulikutwa na nyaraka ambazo
ndizo zilizosababisha mwili huo utambuliwe kuwa ni wa Amelia Rapodile. Askari wa
upelelezi walipofuatilia mahali alipokuwa akifanya kazi, wafanya kazi wenzie
walidai kwamba alikuwa na miadi na mtu aliyemtaja kwa jina la Moses Sethole
mnamo Septemba 7. Hiyo ndiyo siku aliyotoweka.
Polisi pia walikuta barua ya maombi ya kazi kwenye
taasisi ya Sethole iliyotajwa kwa jina la Youth Against Human abuse
organization, ambapo alikuwa amemwahidi kumuajiri Amelia.Walipofuatilia kwa
kutumia namba za simu zilizokutwa kwenye maombi ya kazi walikutana na mwanamke
alijitambulisha kwa jina la Kwazi Sithole anayeishi katika eneo la Wattville
kusini mwa mji wa Boksburg. Alikuwa ni dada yake Moses.
Lakini aliwambia askari wa upelelezi kwamba Sithole
haishi pale na hajulikani mahali alipo.Kuanzia hapo askari wa upelelezi wakajua
kwamba wanaye mtu sahihi aliyehusika na mauaji hayo na si mwingine bali ni Moses
Sithole.Kutokana na taarifa za mauiaji hayo kusambaa nchi nzima, na kuleta hofu
miongoni mwa jamii ya wa Afrika Kusini, Polisi walitangaza zawadi nono kwa mtu
yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea muuaji huyo
kukamatwa.
Pia aliyekuwa raisi wa chi hiyo wakati huo Nelson
Mandela aliingilia kati jambo hilo na kuwahimiza Polisi wakakikishe muuaji
anakamatwa haraka iwezekanvyo na kurejesha utulivu kwa wananchi wa nchi hiyo
ambao walikuwa wametaharuki kutokana na mauaji hayo.
Mnamo Octoba 3, mtu mmoja alipiga simu katika gazeti
maarufu la The Star la nchini humo na kuongea na mwandishi wa habari
aitwae Tamsen de Beer.
Mtu huyo alijitambulisha kwa jina la Joseph
Mangwena na alidai kwamba ndiye anayehusika na mauaji Gauteng (Gauteng ni jimbo
yalipo majiji la Johannesburg na Pretoria). Kwa kauli yake mwenyewe mtu huyo
alisema kwa utulivu. “Mimi ndiye mtu ninayetafutwa kwa udi na uvumba.”
Alisema kwamba anataka kujisalimisha. Mwandishi huyo wa habari aliwasiliana na
Polisi.
Mtu huyo alipiga simu mara kadhaa katika ofisi za
gazeti hilo na simu yake ilirekodiwa. Na katika maelezo yake kwa mwandishi huyo
wa habari alieleza kwa undani jinsi alivyotekeleza mauaji hayo. Alidai kwamba
alianza kuuwa baada ya mwanamke mmoja kumtuhumu kimakosa kwamba alimbaka ambapo
alishitakiwa na kuhukumiwa kwenda jela. Wakati alipokuwa jela aliteswa sana na
wafungwa wenzake. “Nilipotoka niliamua kulipiza kisasi.
Nilikuwa namlazimisha mwanamke ninayetaka kumuuwa
kwenda mahali ninapotaka na tunapofika hapo ninamwambia, ‘Unajua kwa
nini?’ Niliteseka sana na sasa ni wakati wangu kulipiza kisasi, na ndipo
huwauwa.”
Alisema mtu huyo katika mazungmzo yake kwa njia ya
simu na mwandishi huyo wa habari. Alisema kwamba alikuwa anatumia nguo za
wahanga wake kuwanyongea na alikuwa anapendelea chupi zao kwa sababu haziachi
alama za vidole. Aliendelea kusema kwamba baadhi ya wanawake aliowauwa walikuwa
wakishuhudia maiti za wenzao aliowaua na kutelekeza miili yao mahali
hapo.
Hata hivyo alikanusha kuhusika na mauaji ya Letta
Ndlangamandla na mwanaye wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 2. Alidai kwamba
yeye anawapenda watoto hivyo asingeweza kumuua mwanamke huyo wala mtoto
wake.Alielezea mahali alipotelekeza miili mingine ambayo Polisi walikuwa
hawajaiona. Kutokana na maelezo hayo waliamini kwamba huyo ndiye muuaji
waliyekuwa wakimtafuta.
Hata hivyo kutokana na ugumu wa kumpata huyo muuaji
aliyepiga simu, askari wa upelelezi waliamua kuendelea kumtafuta mtuhumiwa
wanayemfahamu Moses Sethole. Walitoa picha zake kwenye magazeti hapo mnamo
Octoba 13, na waliwaomba wananchi wasaidie kupatikana kwa mtu
huyo.
Siku chache baada ya
picha yake kuwekwa magazetini, Sithole aliwasiliana na shemejie aliyemuoa dada
yake akimuomba amtafutie bunduki ya kujilinda.
Walikubaliana na shemejie
wakutane kwenye eneo la viwanda la Mintex lililopo katika mji wa Benon ambapo
atapewa hiyo silaha. Dada yake aliwasiliana na Polisi na kuwaeleza kuhusu ombi
la Sithole kwa shemejie la kutaka atafutiwe silaha ya kujilinda. Kapteni
Vinol Viljoen na Frans van Niekerk waliona huo ndio wakati muafaka wa kumtia
muuaji huyo mbaroni.
Walikutana na uongozi wa kiwanda na kukubaliana kuwa
Inspekta Francis Mulovhedzi ajifanye ni mlinzi wa kiwanda akae getini. Ilipofika
saa 9 usiku mnamo Octoba 18, 1995, Sithole aliwasili na kumuulizia Maxwell.
Askari aliyekuwepo getini alimwambia Inspekta Mulovhedzi aende kumtafuta Maxwell
ndani ya kiwanda.
Kwa kuwa alikuwa ni mgeni pale na hakutaka
kumuachia Sithole aondoke, alikataa kwenda ndani kumtafuta Maxwell, jambo hilo
lilileta ubishani kidogo na hivyo kumfanya Sithole ajenge wasiwasi na kukimbia
kutoka katika eneo hilo.Inspekta Mulovhedzi alimfuata kule gizani alipokimbilia.
Alijitambulisha kama Afisa wa Polisi akimpigia Sithole kelele asimame na kupiga
risasi mbili hewani.
Pamoja na kwamba katika mazungumzo yake kwa njia ya
simu na mwandishi wa habari alidai kwamba anataka kujisalimisha, lakini
hakujisalimisha kirahisi kama ilivyotarajiwa. Alimjia yule Polisi akiwa na
shoka. Ili kujihami askari huyo alimpiga risasi ya miguuni hata hivyo pamoja na
kupigwa risasi lakini aliendelea kutaka kumpiga askari huyo na shoka ambapo
alimpiga tena risasi ya miguuni mpaka akaanguka.
Alikuwa amepigwa risasi ya miguuni na tumboni hivyo
alikimbizwa katika hospitali ya Glynwood iliyoko Benoni ambapo alifanyiwa
upasuaji siku iliyofuata.
Wakati Brigedia Suike Britz Kamanda wa kitengo cha
mauaji na ujambazi wa kutumia silaha alipopata taarifa za Sithole kupigwa
risasi, moyo wake ulisimama kwa sekunde kadhaa kwa mshtuko. Baadaye akizungumzia
tukio hilo alisema,
“Ilikuwa kama déjà vu kutokana na kufanana
kwa usahihi kabisa na tukio la kuuawa kwa David Selepe, tukio ambalo hadi sasa
vyombo vya habari vimelishupalia wakitushutumu kwa uzembe. Nilisali wakati wote
nikihofu kwamba Sithole naye angekufa na nilikuwa napiga simu kila saa ili
kufuatilia hali ya afya yake.” (Déjà vu ni kitendo cha kufanana kwa jambo
au matukio).
Hata hivyo Sithole alipata nafuu na hivyo
kuhamishiwa katika hospitali ya kijeshi iliyoko katika jiji la Pritoria, ambapo
ulinzi uliimarishwa.
Habari ya kukamatwa kwa Moses Sithole zilisambaa
nchini humo kama moto wa mwituni.Mnamo Octoba 28 magazeti nchini humo yaliripoti
kwamba Sithole alikutwa na Maradhi ya Ukimwi (HIV), hata hivyo Polisi hawakutoa
maoni yao kuhusiana na taarifa hizo. Ilidaiwa kwamba kuna uwezekano maradhi hayo
aliyapata kutoka kwa mmoaj wa wahanga wake aliowabaka na
kuwauwa.
Wakati huo huo askari wa upelelezi Viljoen na Frans
Van Niekerk walimtembelea Sithole hospitalini kwa ajili ya kumuhoji, lakini
alikuwa mkaidi kujibu maswali yao. Alipoingia askari mwanamke kumuhoji alikiri
baadhi ya mauaji aliyoyafanya na kitendo cha kupiga punyeto kwenye miili ya
wanawake hao baada ya kuwauwa. Mahojiano hayo yalirekodiwa.Kwa maneno yake
mwenyewe Sithole alisema.
“katika eneo la Atterdgeville niliuwa wanawake labda
kumi hivi, siwezi kukumbuka kwa usahihi, nilikuwa nawakamata kwa mikono yangu
shingoni na kuwanyonga na wakati mwingine nilikuwa natafuta kitu kama kamba ya
kuwanyongea. Nilikuwa natumia soksi ya viatu na kuwafunga shingoni na kisha
kuwanyonga. Mimi sipendi kuona damu. Nilikuwa nawalazimisha kulala kifudifudi
wakati nikiwabaka na baada ya kufanya hivyo nawanyonga na wakati nikiwaangalia
wakifa, napiga punyeto juu ya miili yao.
”Sithole alikanusha
kushirikiana na mtu yeyote katika kutekeleza mauaji hayo lakini alisema kwamba
kuna uwezekano kuna mtu mwingine aliyekuwa akifanya mauaji sambamba na yeye.
Mnamo Novemba 3, Sithole aliruhusiwa kutoka hospitalini na kupelekwa
katika jela ya Boskburg, jela ambayo aliwahi kufungwa wakati fulani kwa kosa la
kubaka.
Jela hiyo iko jirani kabisa na eneo alilokuwa
akiitelekeza miili ya wanawake aliokuwa akiwauwa.Baadae aliwapeleka Polisi
sehemu mbalimbali ambazo alitelekeza miili ya wanawake wengine aliowauwa ambapo
baadhi ya sehemu hizo hazikupata kujulikana na polisi.
Mnamo Mei 20, Sithole alifikishwa mahakamani kwa
mara ya kwanza na baada ya kusomewa mashitaka kesi iliahirishwa mpaka baaba ya
miezi mitano ndipo itakapoanza kusikilizwa rasmi. Alikuwa akitetewana wakili wa
kujitegemea aitwae Eben Jordaan ambapo gharama za kumtetea zilibebwa na serikali
ya Afrika ya Kusini.
Mnamo Octoba 28, Moses Sithole alifikiswa mahakamni
na kusomewa mashikiwa kwa makosa mauaji ya wanawake 38 akiwemo mtoto mmoja wa
miaka 2, makosa 40 ya ubakaji na makosa 6 ya uporaji wa kutumia silaha. Sithole
alikanusha mashitaka hayo.
Mnamo Desemba 5, 1997, Sithole alihukumiwa cha miaka
50 kwa kila kosa la mauaji ya wanawake 38, miaka mingine 12 kwa kila kosa la
ubakaji wa wanawake 40 na miaka 5 kwa kila kosa la ujambazii wa kutumia silaha.
Kwa kuwa kifungo cha makosa hayo kitaenda pamoja, alitakiwa atumikie kifungo cha
miaka 2,410. Mheshimiwa Jaji David Carstairs aliagiza
atumikie angalau kifungo cha miaka 930, ndipo afikiriwe kupewa fursa ya
kutumikia kifungo cha nje (Parole).
Post a Comment