Waziri
wa Fedha Dkt .William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki
Okada(kulia)wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu
ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili
ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar
es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini.
Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli(katikati)
Waziri
wa Fedha Dkt .William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki
Okada(kulia)wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu
ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili
ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar
es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini.
Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli(katikati)
Balozi
wa Japan nchini Masaki Okada(kulia) akizungumza na waandishi wa habari
jana (leo) mjini Dodoma mara baada yake kusaini na Tanzania hati ya
makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania
shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu
katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine
zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni Waziri wa Fedha Dkt
.William Mgimwa (katikati) na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli(kushoto) Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori
Onishi(kulia) akielezea mkakati watakaoutumia katika ujenzi wa daraja
la juu katika makutano ya TAZARAjana(leo) mjini Dodoma wakati wa sherehe
za kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan
itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa
barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam
na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ( wa pili kutoka kulia) , Waziri wa
Fedha Dkt William Mgimwa (wa pili kushoto) na Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli(kushoto)
Waziri
wa Fedha Dkt .William Mgimwa (katikati ) na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori Onishi(kulia)wakisaini
hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha
Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa
juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine
zitasaidia katika kupunguza umaskini. Sherehe zilifanyika jana (leo)
mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli(kushoto)
Waziri
wa Fedha Dkt .William Mgimwa (katikati ) na Balozi wa Japan nchini
Masaki Okada(kulia)wakisaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu
ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili
ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar
es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini.
Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto) Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori
Onishi(kulia) na Waziri wa Fedha wakibadilishana hati ya ujenzi wa
daraja la juu katika makutano ya TAZARAjana(leo) mjini Dodoma wakati wa
sherehe za kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo
Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa
barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam
na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ( kulia) , na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli(katikati)
Dr.
Magufuli—Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto) akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari jana(leo) mjini Dodoma juuu ya juhudi za
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ya kupunguza msongamano katika Jiji la
Dar es salaam ambapo jana (leo) Tanzania imepata mkopo wa shilingi
bilioni 52.5 kutoka Japan kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika
makutano ya TAZARA. Wengine ni Waziri wa Fedha Dkt . William
Mgimwa(katikati) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada(kullia)
Picha na GCU-HAZINA_Dodoma
Na Mwandishi wetu_GCU–HAZINA-Dodoma
Tanzania
na Japan zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa mkopo wenye riba
nafuu wa kuikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ya
kutekeleza shughuli za maendeleo hapa nchini.
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo(jana) mjini Dodoma ambapo kwa Tanzania
iliwakilishwa na Waziri wa Fedha Dkt .William Mgimwa na Balozi wa Japan
nchini Masaki Okada.
Akizungumza
mara baada ya kutiwa kwa saini makubaliano hayo Waziri wa Fedha Dkt.
Mgimwa alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 52.5 zitatumika
katika ujenzi wa barabara ya juu kwa juu(daraja) katika makutano ya
TAZARA jijini Dar es salaam .
Aliongeza
kuwa kiasi kilichobaki ya shilingi bilioni 25.2 zitatumika katika
kupunguza umaskini kwa fedha hizo kuingizwa katika Mfuko wa Bajeti(
General Budget Supoort-GBS) .
Dkt.
Mgimwa alisema kuwa mkopo huo umetolewa kwa masharti nafuu ambapo riba
yake ni asilimia 0.01 na utalipwa kwa kipindi cha miaka 30 ambapo
Tanzania itaanza kuulipa baada ya miaka 10 kutoka sasa.
Naye
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi
wa daraja la juu katika makutano ya TAZARA utasaidia kupunguza
msongamano katika Jiji la Dar es salaam na hivyo kupunguza muda wa
watumiaji wa barabara za Jiji hilomkukaa katika foleni.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuwa wananchi
wa Dar es salaam watakuwa na muda mrefu wa kufanya kazi kuliko kukaa
katika foleni.
Naye
Waziri wa Ujenzi Dkt. Jphn Magufuli alisema kuwa daraja hilo litakuwa
na urefu wa Kilometa 1.2 na kuongeza kuwa kukamilika kwake itakuwa hatua
mkombozi kwa wakazi wa Dar es salaam.
Alisema
kuwa Serikali itaendelea kuboresha barabara mbalimbali za jiji la Dar
es salaam ili kuhakikisha kuwa foleni katika mji huo zinapungua .
Aidha
Dkt. Magufuli alitoa siku saba kwa wakazi walioko kandokando ya
barabara ya Mwenge Morocco kubomoa nyumba zao zilizoko katika hifadhi ya
barabara kabla Serikali hajaanza kutekeleza zoezi hilo kwa nguvu.
Alisema
kuwa kimsingi wananchi wa eneo hilo walishalipwa fidia hivyo hawana
sababu ya kuchelewesha upanuzi wa barabara hiyo ambapo inasababisha
foleni kwa watumiaji.
Post a Comment