Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akisalimiana na
Mafisa wa kikosi cha 842 kambi ya JKT Mlale kabla ya kufunga mafunzo
.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto
akiongozwa na kamanda wa gwaride Meja Bosco Singambele kwenda kukagua gwaride la
vijana wa mujibu wa sheria na aliye nyuma ni mkuu wa kikosi cha 842 JKT Mlale
Meja Thomas Mpuku
Meja Bosco Singambele akiongoza gwaride lililoandaliwa
na kupita mbele ya jukwaa na kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya JKT wakila kiapo baada
ya kuhitimu mafunzo waliyokuwa wakifanya katika kikosi cha 842 cha JKT
Malale
Hawa nao wakila viapo vyao
Wahitimu wakisikiliza nasaha toka kwa mgeni Rasmi
baada ya kumaliza gwaride
Mkuu wa Kikosi cha 842 JKT Mlale Meja Thomas Mpuku
akizungumza wakati wa sherehe hizo,katikati mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu nawa pili kuliaMkuu wa Wilaya ya Songea Joseph
Mkirikiti
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa nasaha
zake kwa vijana wa operesheni miaka 50 ya uhuru katika kikosi cha 842 JKT MLALE
, katikati ni mku wa kikosi hicho Meja Thomas Mpuku na kushoto ni Luteni kanal
Menance Mbele
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya
tsh 50,000 kwa kiongozi wa kikundi cha singe ambacho kilifanya vizuri wakati wa
sherehe ya kufunga mafunzo hayo
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wa tatu kutoka
kushoto,akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
ya mkoa wa Ruvuma,wa pili kushoto Luten Kanal Menance Mbele kutoka makao makuu
ya JKT na mkuu wa utumishi, wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Songea Joseph
Mkirikiti na wa tatu kulia mkuu wa kikosi cha 842 JKT Mlale Meja Thomas
Mpuku
------------------------------------------------
Na YEREMIAS
NGERANGERA.....SONGEA
Mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga
taifa JKT kwa mujibu wa sheria ya operesheni ya miaka hamsini ya
jeshi la kujenga taifa waliohitimu katika kikosi cha 842 cha Mlale wilayani
Songea mkoani Ruvuma yamehitimishwa kwa wahitimu hao kutakiwa kuyatumia
mafunzo hayo waliyoyapata kwa maslahi ya taifa zaidi na siyo kujihusisha na
vitendo viovu.
Akizungumza kabla ya kufunga mafunzo hayo mkuu wa mkoa
wa Ruvuma Said Mwambungu aliwataka wahitimu hao 377 kuhakikisha kuwa wanakuwa
mfano katika jamii kwa sababu wao ni miongoni kwa wanafunzi waliopata mafunzo
hayo ya awali ya kijeshi huku wakiwa wametoka shuleni ambako wamesemoma
mambo mbali mbali lakini kubwa likiwa ni uzalenzo
kwa nchi yao ambao unahitajika na kila mmoja kwa mustakabali wa
taifa.
Amesema kuwa wanapaswa kuwa tofauti na na vijana wenzao
wa mitaani kwa sababuwao ni wasomi ambao ni kioo cha jamii hivyo
uaminifu,uadilifu na ustahimilivu iwe ni dira kwao kwa sababu serikali imeamua
kurudisha mafunzo hayo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria hivyo wanapaswa kuelewa
kuwa nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ambazo kila mmoja anapaswa kuzitii
hivyo wao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika
kikosi hicho ambazo ni bara bara,umeme na maji Mkuu wa mkoa alisema kuwa mambo
hayo yote yatafanyiwa kazi huku suala la maji kikosini hapo
akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Songea
na mkuu wa kikosi hicho kuona uwezekano wa kulitatua huku suala
ajira kwa wahitimu hao akisema kuwa serikali haiwezi kuwaacha wahitimu wote
waishie kuzagaa mitaani ingawa pia haiwezi kutoa ajira kwa
wote.
Awali akizungumza mwakilishi wa mkuu wa jeshi la
kujenga taifa nchini Luteni Kanali Mbele alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ya
awali ya kijeshi ni kuwajengea moyo wa uzalendo kwa taifa na kulitumikia kwa
uadilifu na siyo vinginevyo kwa sababu baadhi ya wahitimu wamekuwa wakiyatumia
mafunzo hayo kufanya uhalifu na vitendo vingine vya uvunjifu wa
amani.
Aliwaasa wahitimu hao wa mafunzo ambao kati yao
wavulana ni 302 na wasichana ni 75 huku akisema kuwa wa wanafunzi
wanne walishindwa kuendelea na mafunzo kwa sababu ya utoro na ugonjwa kwa mmoja
ambaye anaendelea na matibababu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili
na kuwataka wale ambao baada ya kuhitimu mafunzo hayo wanakwenda
kuendelea na masomo katika vyuo mbali mbali kujiepusha na migomo
na ukiukwaji wa sheria na wanapaswa kutambua kuwa fedha zinazotumika kuwasomesha
zinatokana na kodi za wazazi wao hivyo si busara kushirikia katika vitendo viovu
vya kuanzisha au kushiriki migomo vyuoni shuleni au mitaani kwa kisingizio kuwa
wao wamepata mafunzo ya kijeshi wana haki ya kufanya kitu chochote
.
Aidha aliwataka kuacha tabia ya kuzagaa mitaani na
kujihusiaha na tabia ambazo si utamaduni wa taifa ambalo limejengwa katika
misingi ya amani na utulivu pamojana uadilifu kwa miaka mingi hivyo ni wajibu
wao kudumisha hayo yaliyoasisiwa na waasisi wa taifa hili
Post a Comment