Siku
chache baada ya mchezaji Mrisho Khalfan Ngasa kusajiliwa na klabu ya
Yanga akitokea klabu ya Simba ambako alikuwa anacheza kwa mkopo toka
klabu ya Azam fc shirikisho la soka Tanzania limeubatilisha mkataba
uliopo baina ya Ngassa na Yanga ikisema kuwa haujasajiliwa kwenye ofisi
zake .
Shirikisho limezungumza hayo mwishoni mwa wiki hii kupitia
kwa msemaji wake ambaye ni Afisa habari wa TFF Boniface Wambura ambaye
alisema kuwa TFF inautambua mkataba uliopo baina ya Simba na Ngassa na
si wa Ngassa na Yanga kwa kuwa haujasajiliwa na uliosajiliwa TFF ni
mkataba wa Simba unaoonyesha kuwa Ngassa ataitumikia Simba msimu ujao
kwa muda wa mwaka mmoja .
Ngassa amekuwa akizua gumzo kwenye masuala ya usajili tangu
aliposajiliwa toka Yanga kwenda klabu ya Azam na baada ya hapo akahamia
Simba kwa mkopo kabla ya kurudi Yanga . Viongozi wa Simba awali
walisikika wakisema kuwa Ngassa ni mchezaji wao halali na sheria za
usajili za TFF zitachukua mkondo wake jambo ambalo linaonekana
kudhihirika .
Kanuni za TFF kuhusiana na masuala ya usajili wa wachezaji
zinasema kuwa lazima mkataba wa mchezaji husika usajiliwe kwenye ofisi
za TFF . Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa mkataba wa
Ngassa na Yanga haujafika TFF na ndio maana hata kwenye timu ya Taifa ,
Taifa Stars ameorodheshwa kama mchezaji wa Simba.
Bado viongozi wa Yanga na Simba pamoja na mhusika mkuu kwenye
sakata hili Mchezaji mwenyewe hawajatoa tamko lolote juu ya taarifa hii
ya Tff kutotambua mkataba wa Ngassa na Yanga.
Burhan awekewa vikwazo na Marekani
7 hours ago
Post a Comment