NAIBU Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Agrey Mwanri, Jumapili 8, 2013, amechangisha Milioni 8 katika
Harambee ya Ujenzi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Bwigiri Usharika wa Chamwino.
Mwanri
alitumia Nusu Saa kuendesha Harambee hiyo kutokana na kuwa na Majukumu
mengine, alichangia Sh. Milioni Moja,ambapo aliahidi, atawasilisha
Michango ya watu watakaomuunga Mkono aliowapelekea Kadi za Ombi la
Mchango huo.
Katika
Harambee hiyo Fesha Taslimu zilikuwa Mil. Tatu ambapo ahadi zilikuwa
Mil. Nne, na fedha zingine zilitokana na Mauzo ya Vitu mbalimbali
vilivyochangwa kwenye Harambee hiyo na kubadilishwa kuwa fedha baada ya
kuuzwa kanisani hapo.
Harambee
hiyo ambayo ilihusisha Sharika Zote za KKKT Dayosisi ya Dodoma,
ilihudhuriwa na Wachungaji wote wa Kanisa hilo mkoani humo, ambapo
wachungaji wachache ambao hawakuhudhuria waliwakilishwa na Viongozi wa
Juu wa Sharika hizo.
Kaimu
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya hiyo, Samwel Mshana, alikuwa mmojawapo wa
wageni waalikwa katika Harambee ya Mtaa huo wa KKKT Bwigiri, ambapo
wengine walikuwa ni pamoja na Mkuu wa Jimbo la Makao Makuu Dodoma,
Jackson Sharua.
Hata
hivyo Sharika mbali ziliwasilisha Michango yake kwenye Mtaa huo, ili
kufanikisha Ujenzi wa Nyumba ya kuabudia, ambapo kwa muda Mrefu Waumini
wa Kanisa hilo walikuwa wakiabudia kwenye Nyumba ya Mzee wa Kanisa,
Maiko Msuya anayeipenda KKKT.
Aidha
Kaimu Askofu Mshana, Mchungaji wa Usharika wa Chamwino Greyson Mhoka na
Mwinjilisti wa Mtaa wa Bwigiri Rizikiel Shekivuli, kwa niaba ya
Washarika, walimshukuru Waziri Mwanri kwa kuona Umuhimu wa kulisaidia
Kanisa la KKKT Bwigiri na Washarika wa Chamwino ili wawe na Mahali pa
kuabudia, badala ya kuabudia nje kwa muda mrefu.
Post a Comment