- IGP Mwema
- ...................................................
Na Elizabeth Ntambala
Rukwa
POLISI mkoani Rukwa inamtafuta mwanaume mmoja aitwae Amos Ukiwa (33) kwa tuhumu ya mauaji ya mke wake pamoja na mwanae,waliofariki juzi katika wilaya ya sumbawanga vijijini.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jakobo Mwalwanda alisema kuwa mauaji hayo
yalitokea usiku wa kuamkia Juni 24 majira ya saa sita usiku huko katika
kijiji cha momba wilaya ya sumbawanga vijiji na kudaiwa kuwa chanzo cha
mauaji ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda Malwanda alimtaja mama aliyeuawa kuwa ni Happy Lucas (25)pamoja na mwanaye wa miezi mitano aitwaye Bakari Ukiwa ambao walichomwa visu na mumewake wakiwa nyumbani
kwao ile hali baada ya majibizano ya hapa na pale mama alijikuta akiwa
katika wakati mgumu na kuanza kupata kipigo kutoka kwa mwanaume huyo
asiyekuwa hata na huruma na mwanaye.
Inadaiwa kuwa chanzo cha mauji hayo yaliyotokea nyumbani kwa wanandoa hao, ulitokana na wivu wa kimapenzi kwani mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu mkewe akisaliti ndoa
yao.

on Tuesday, June 25, 2013
Post a Comment