Rais
Mahinda Rajapaksa (katikati) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii
Balozi Khamis Kagasheki (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Butiama
Anjelina Mabula mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa
Serengeti.
Rais Mahinda Rajapaksa akiaga mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Serengeti tayari kwa safari ya kurejea Dar es Salaam
………………………………………………..
Rais
wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa ambaye yuko nchini kuhudhuria Mkutano wa
Global Smart Partneship jana alitembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na
kuvutiwa na mandhari nzuri ya Serengeti iliyosheheni wanyama mbalimbali.
Rais Rajapaksa aliwasili asubuhi jana na kufanya safari ya utalii wa
siku (day trip) akiwa amefuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi
Khamis Kagasheki. Katika muda mfupi aliotembelea Serengeti aliweza
kujionea wanyama mbali mbali kama vile Simba, Tembo, Twiga na makundi
makubwa ya pundamilia na nyumbu.
Aidha,
kufuatia kuvutiwa na uzuri wa Serengeti Rais Rajapaksa aliahidi
kutembelea tena hifadhi hiyo mwezi ujao akiwa na familia yake ili waweze
kujionea uzuri wa hifadhi hiyo akiwa na muda wa kutosha pamoja na
familia yake.
Post a Comment