Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanzania yaahidi kuendelea kuunga mkono hatua za Kimataifa za kutafuta amani kati ya Palestina na Israel pamoja na Mashariki ya kati kwa ujumla.

 

209
KiongoziwaUjumbewa Chama cha Ukombozi wa Kipalestina Taysear Ishled akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kumaliza mazungumzo yao.
197
Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) pamoja na wenyeji wao wa Chama cha Mapinduzi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya PLO ambaye ni Kiongozi Taysear Ishaled, Saleh Raafat na nyuma yao ni Balozi wa Palestina Tanzania Nasri Abujaish. Kulia ya Balozi ni Katibu wa Sekriterieti ya CCM uhusiano wa Kimataifa Balozi Asha Rose Migiro.
205
Katibu wa Sekriteriet ya CCM Uhusiano wa Kimataifa Balozi AshaRose Migiro akiteta jambo na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya Ugeni wao kutoka Chama cha Kipalestina kuonana naye.
333
Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dkt. Ad Koekkoek akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kumaliza muda wake wa utumishi Nchini Tanzania ifikapo Mwezi Julai mwaka huu wa 2013.
365
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpatia zawadi ya Kasha Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dkt. Ad Koekkoek kama ishar ya ukumbusho kutokana na utumishi wake mzuri hapa Tanzania.(Pichana Hassan Issawa – OMPR – ZNZ).

Serikali ya Uholanzi imeipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuifungua tena ofisi yake ya Ubalozi iliyopo Nchini Uholanzi kitendo ambacho kitazidisha uhusiano wa karibu kati ya Mataifa hayo mawili.
Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dkt. Ad Koekkoek wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Dkt. Koekkoek ambae amekuja kuaga akikaribia kumaliza muda wake wa utumishi wa Kidiplomasia akiiwakilisha Nchi yake ya Uholanzi katika Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amesema uamuzi wa Tanzania wa kufungua Ofisi hiyo umekuja wakati muafaka kutokana na muingiliano wa Kiuchumi wa pande hizo mbili.
Alitolea mfano wa muingiliano huo kuwa ni ile ziara ya Ujumbewa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliyoifanya hivi karibuni kutembelea Nchi hiyo na hatimae kuzaliwa wazo la Wataalamu wa Kampuni ya Mafuta ya Shell kushawishika kuja Visiwani kutoa Taaluma katika masuala ya Mafuta na Gesi.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amempongeza Balozi huyo wa Uholanzi Nchini Tanzania Dkt. Ad Koekkoek kwa utumishi wake makini uliopelekea kuimarika zaidi kwa uhusiano kati ya Mataifa hayo mawili rafiki.
Balozi Seif amesema fursa kadhaa za masomo wanazoendelea kupatiwa Wanafunzi wa Kitanzania Nchini Uholanzi katika Fani tofauti ni ishara ya juhudi za Balozi huyo anayetarajiwa kumaliza muda wake mwezi ujao wa Julai Mwaka huu wa 2013.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi Watatu wa Chama cha Ukombozi wa Kipalestina ( PLO) ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho TaysearIshalied.
Katika mazungumzo hayo Balozi Seif ameueleza Ujumbe huo kwamba Jamuhuri ya Muunganowa Tanzania itaendelea kuunga mkono hatua za Kimataifa za kutafuta amani kati ya Palestina na Israel pamoja na Mashariki ya kati kwa ujumla.
Baadaye Ujumbe huo wa Viongozi watatu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina ( PLO)ulikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Pandu Ameir Kificho na kubadilishana mawazo juu ya uhusiano wa karibu wa pande hizo mbili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top