Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIGOGO 200 WAHOJIWA MABILIONI YA USWISI ... VIGOGO WENYEWE NI HAWA HAPA ....

 


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

DAR ES SALAAM. 
SUALA la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
        
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.

Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatar
ajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Jaji Werema alipoulizwa na Mwananchi Jumpili maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.
           
“Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.

“Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.”

Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa.

Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.

Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.

Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini.

Werema anaripotiwa akiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta.

Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.
CHANZO MWANANCHI.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top