Issa
Bakari ama Mr. Big alizungumza kwa niaba ya wachinjaji wa songea kufuatia kubomolewa kwa mazizi ya kuhifadhia ng'ombe.
Mwenyekiti wa
umoja wa wachinjaji wa ng’ombe wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni diwani wa
kata ya Misufini Salum Mfamaji akitoa kero zake kwa waandishi wa habari waliojitokeza katika tukio hilo usiku huu.
Diwani
wa
kata ya Msamala Bw.Mgwasaakizungumza na wafanya biashara kutafuta
muafaka ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza kwa kesho
kutokana na mgomo huo
Huu ni umati uliuokusanyika wa wachinjaji wa ng’ombe pamoja na wamiliki na wafanyabiashara wa Manispaa ya Songea wakijadili kubomolewa mazizi yao
Hawa
ni ng'ombe ambao wamebomolewa mazizi yao na sasa wametapakaa katika
uwanja na kuwafanya wafanyabiashara kukesha usiku huu kwa kuwalinda ili
waipotee na kusababisha hasara
...................................................
Na Nathan Mtega,Songea
WAKAZI wa mji wa Songea mkoani Ruvuma wako hatarini
kukosa kitoweo cha nyama ya ng’ombe kufuatia mgomo uliotangazwa na wachinjaji
hao wa ng’ombe pamoja na wamiliki na wafanyabiashara baada ya mazizi ya
kuhifadhia mg’ombe yaliyopo katika machinjio ya kata ya Msamala mjini Songea
kuvunjwa kwa amri ya uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea bila wao
kujulishwa kuhusisana na hatua hiyo.
Wakizungumza na
waandishi wa habari wachinjaji hao zaidi ya mia mbili muda mfupi baada ya tukio
hilo la kuvunjwa kwa mazizi hayo ya machinjio wakiongozwa na Issa Bakari
walisema kuwa kulikuwa na mpango wa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya
Songea kuhamisha machinjio hayo na kuyapeleka katika kata ya Tanga kwenye
kitongoji cha Masigila ambao ulikuwa bado haujaanza kutekelezwa.
Akizungumza Issa
Bakari kwa niaba ya wachinjaji wenzake alisema kuwa eneo hilo ambalo linaelezwa na uongozi wa Manispaa
kuwa ndiko ambako wachinjaji wanapaswa kuhamishiwa kwa shughuli hizo bado
hakujaandaliwa na hakuna miundo mbinu ya kukidhi ikiwemo vyoo pamoja na
mazingira ya kuwatunzia ng’ombe hao kabla ya kuchinjwa.
Alisema kuwa wao
hawajakataa uamuzi huon lakini walipaswa kushirikishwa kwa kila hatua ya
utekelezaji badala ya kuvunja mazizi huku ng’ombe wakiwepo na hawajui hatma ya
ng’ombe wao ambao hawatakuwa na msahali pa kuhifadhiwa kabla ya kuchinjwa na
tukio hilo
limefanywa usiku wa Juni 4 majira ya saa 1;30 usiku bila taarifa.
Akizungumza diwani wa
kata ya Msamala Bw.Mgwasa alisema kuwa yeye ni miongoni mwa madiwani wa
halmashauri ya Manispaa ya Songea lakini hakuna kikao kilichoketi na kufikia
maamuzi hayo ya kuvunja mazizi hayo hali ambayo inapaswa kulaaniwa na kila
mmoja huku akiwasihi wachinjaji hao kutositisha huduma hiyo muhimu kwa wananchi
na suala hilo litafanyiwa kazi kazi mara moja na kutadutiwa ufumbuzi bila
kuwaathiri wafanyabiashara hao pamoja na wananchi kwa ujumla.
Naye mwenyekiti wa
umoja wa wachinjaji wa ng’ombe wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni diwani wa
kata ya Misufini Salum Mfamaji mbali ya kusisitiza kuwa huenda huduma hiyo
ikasitishwa kuanzia kesho lakini aliwaomba wachinjaji hao kuwa na subira wakati
viongozi wao wakiendelea kutafuta ufumbuzi kwa kufuata taratibu za halmashauri
ya Manispaa ya Songea.
Post a Comment